Waziri wa Vijana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Marekani washuhudia Utiaji saini wa itifaki kati ya Chuo Kikuu hicho na Shirikisho la Al-khomasi ili kuandaa michuano ya Kombe la Dunia


DkT. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na DkT. Ahmed Dalal, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo, walishuhudia sherehe ya utiaji saini wa itifaki kati ya Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo na Shirikisho la Misri la  Al-khomasi la Kisasa , Misri itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Al-khomasi la Kisasa katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Marekani huko  Kairo mpya. 


Misri itakuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia la Al-Khomasi la Kisasa  kuanzia tarehe 20 hadi 28 Machi 2022, na kushirikisha wachezaji 200 wa kiume na wa kike wakiwakilisha nchi 35.


 DkT. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alimshukuru DkT. Ahmed Dalal, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo, kwa kuandaa Kombe la Dunia la Al-Khomasi la Kisasa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu cha Marekani. 


Alisifu kina ya mahusiano na ushirikiano unaoendelea unaounganisha Wizara ya Vijana na Michezo na Chuo Kikuu cha Marekani katika nyanja nyingi. 


Kwa upande wake, DkT Ahmed Dalal, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo, alieleza furaha yake kwa kuandaa Kombe la Dunia la Al-Khomasi la Kisasa kwenye viwanja vya Chuo Kikuu hicho. 


Akisisitiza kuwa Chuo Kikuu hutoa uwezekano wote kwa Ushirikiano na Shirikisho la Misri la Al-Khomasi la kisasa ili kufanya kazi kwa mafanikio ya mashindano hayo na yawe na mwonekano mzuri kwa jina na Cheo cha kimataifa cha Misri. 


Itifaki hiyo ilitiwa saini na Meja Jenerali Hazem El-Damhougy, Naibu wa Mwenyketi  wa Shirikisho la Misri la  Al-Khomasi la Kisasa na mwakilishi wa Shirikisho hilo, na Bwana Ihab Abd El Rahman, anayewakilisha Chuo Kikuu cha Marekani mjini Kairo. 


Sherehe za Utiaji saini wa itifaki hiyo ilihudhuriwa na Mhandisi Sherif El-Erian, Mwenyketi wa Shirikisho la Misri la Al-Khomasi la kisasa, Dk. Mohamed El-Kurdi, na Abd El Awal Mohamed, Wasaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo kwa Masuala ya Ubingwa, na Mohamed El Domyati, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi . 

Comments