"Wizara ya Vijana na Michezo" yafungua shughuli za mpango wa mafunzo ili kuimarisha na kukuza uwezo wa makada wa Vijana
- 2022-03-17 22:11:14
Mpango huo unalenga kukuza na kuandaa viongozi vijana wa kitaifa ili kuendeleza mchakato wa maendeleo endelevu katika nyanja mbalimbali kulingana na maoni ya siku za Usoni.
Jumamosi Wizara ya Vijana na Michezo, kupitia Utawala Mkuu wa Bunge na Elimu ya Uraia na kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maendeleo ya taifa (Mpango wa Taifa) imefungua mafunzo ya kuandaa wakufunzi “TOT” mpango huo unaolenga kuimarisha na kukuza uwezo wa makada vijana kuchukua nafasi za uongozi na wa kiraia,ili kutoa vijana na wasichana elfu moja kutoka makada na viongozi wa kiraia kuchukua nafasi za uongozi katika uwanja wa kazi ya umma na kugombea kwa kazi ya kiraia, ndani ya mfumo wa kipindi cha pili ya mpango wa "Jukumu Letu", mnamo kipindi cha kuanzia Machi 11 hadi 19, pamoja na ushiriki wa wanafunzi 35.
Hayo yamejiri kwa kuhudhuria Bwana Ahmed Afifi - Mwakilishi wa Wizara na Mkuu wa idhara Kuu ya Bunge na Elimu ya Kiraia, Bibi Randa Al-Bitar - Mkurugenzi Mkuu wa Bunge la viongozi na Vijana, na Dkt. Shaima Al- Qassas - Mwenyekiti wa baraza la idhara ya Jumuiya ya Maendeleo ya taifa.
Mwanzoni mwa hotuba yake, Afifi alisema (Nawasilisha salamu na shauku ya Dkt. Ashraf Sobhy - Waziri wa Vijana na Michezo, na uthibitisho wake thabiti kwamba kukuza makada vijana ni sehemu ya mkakati wa ukuaji wa binadamu)
Akiashiria kuwa maoni ya Waziri ya kubadilisha vituo vya vijana kwa vituo vya huduma kwa jamii yamesababisha utekelezaji wa miradi mingi, mipango ya kijamii na mikutano mbalimbali katika uwanja wa maendeleo ya kijamii, kupitia mpango wa mafunzo makali ili kuzindua mipango kadhaa.
Na aliendelea... kuwa mfumo wa mpango wa mafunzo una mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha ushiriki wa kijamii kwa vijana, kwa kupitia kutengeneza nafasi kubwa za ushirikiano wa ufanisi, kwa kuzingatia uanzishaji na usambazaji wa uanachama (vituo vya vijana, hosteli za vijana, skauti na viongozi, Klabu za michezo).
Dkt.Shaima Al-Qassas alitaja ushirikiano pamoja na Wizara ya Vijana na Michezo unawakilisha ushindi mkubwa na mafanikio muhimu kusaidia wavulana wachipukizi na vijana, kwa kuzingatia uvumbuzi kwa ajili ya maendeleo, akisisitiza kuwa mipango ya ushirikiano na Wizara hiyo inaendelezwa katika nyanja zote.
Alieleza kuwa: "mpango wa mafunzo una mada mbalimbali zinazolenga kuimarisha ushirikiano wa kijamii kwa vijana, kwa kupitia nafasi kubwa zaidi za ushirikiano wa ufanisi, kama ujuzi wa(uongozi - kuandaa kampeni za uchaguzi - utetezi na kupata kuunga mkono - maendeleo ya kijamii - kujenga ushirikiano - hotuba ya umma) .
Bi. Randa Al-Bitar alihitimisha akisema: “Mpango wa mafunzo unafanya kazi ya kuwapa vijana wenye elimu,uzoefu wa kitaaluma na kiutamaduni mbalimbali nafasi ya kufanya kazi pamoja na kubadilishana mawazo yenye manufaa yanayowawezesha kuelewa zaidi mazingira yao ya kijamii na changamoto zinazokabili jamii zao.
Comments