Waziri wa Vijana na Michezo ashuhudia shughuli za Kongamano la kiutamaduni kuhusu "Mabadiliko ya tabianchi na mahusiano yake na masuala ya mwamko"
- 2022-03-19 11:29:22
Dkt. Ashraf Sobhy:
Suala la mwamko ndilo changamoto kubwa zaidi inayolikabili taifa.. ni lazima kuunganisha juhudi zote ili kueneza mwamko kuhusu masuala na changamoto mbalimbali kati ya Wachipukizi na Vijana.
Wizara inaunga mkono mipango ya kuunda kwa Vijana, ambapo tija yake ni kama Kongamano la Utamaduni.
Jumatatu Jioni, Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy alishuhudia shughuli za Kongamano la kiutamaduni linalofanywa na Wizara hiyo kwa ushirikiano na Kongamano la Juni 30 kwa anwani ya "Mabadiliko ya tabianchi na mahusiano yake na masuala ya mwamko" ikiwa ni sehemu ya mpango wa Wizara wa kutoa fursa kwa Vijana kujifunza kuhusu masuala ya mwamko wa jamii, na kueleza maoni yao ya kusaidia kupata ufumbuzi na mitazamo ijayo inayosaidia Nchi katika kukabiliana na masuala hayo.
Programu ya Kongamano la kiutamaduni ilijumuisha mkutano wa mazungumzo uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kituo cha Maendeleo ya Vijana katika Al-Gazira , kwa Mahudhurio ya Dkt. Walid Darwish kama Naibu wa Waziri wa Biashara na Viwanda, Mhandisi Lydia Eleiwa akiwa Naibu Waziri wa Mazingira, Mhandisi Ahmed Abdel Qader kama Mwakilishi wa Waziri wa Rasiliamali za Maji na Umwagiliaji, Dkt. Manal Metwally, Mshauri wa Ulinzi wa Wanyama Pori na Majini wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, na Manaibu kadhaa, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Seneti, na kutoka Wizara ya Vijana na Michezo, Meja Jenerali Ismail El-Far, Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara, Nagwa Salah, Mkuu wa Utawala Mkuu wa Programu za Utamaduni na Hiari, Alaa El-Desouky, Mkurugenzi Mkuu wa Vipindi vya Kiutamaduni na Kisanaa, Dkt. Abdullah Al-Batish, Waziri Msaidizi, Mustafa Magdy, Naibu Waziri, na baadhi ya viongozi.
Kongamano hilo lilijumuisha Utoaji wa Video kuhusu Mabadiliko ya tabianchi, onesho la kisanii la Bendi ya Wizara ya Vijana, inayoongozwa na Maestro Dkt. Mazen Draz, na hotuba ya Mwakilishi Sakina Salameh, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi.
Katika hotuba yake, Dkt Ashraf Sobhy alieleza kuwa Wizara inaunga mkono mipango ya vijana na mawazo ya kuunda, na inatokana na utekelezaji kweli kwa Ushirikiano na pande mbalimbali zinazohusika, na kongamano la Utamaduni liliibuka kwa ushirikiano na kongamano la Juni 30, akionesha kwamba kwa makubaliano na uratibu wa maoni ya Wizara, kongamano hilo la kitamaduni ya kitaifa liliundwa.
Waziri alieleza kuwa wazo la kongamano hilo la kiutamaduni linatokana na mjadala wa vijana, kuwasilisha mawazo kwa mada zenye maslahi kwa nchi, na kujenga hali ya mazungumzo ya kila jambo linalohusu masuala ya jamii, akielekeza Shukrani na kwa pande zote husika na Wizara zinazoshiriki katika shughuli za Kongamano la kiutamaduni.
Pia aliashiria Juhudi za taasisi na Wizara mbalimbali za serikali, haswa Wizara ya Mazingira, kwa uratibu na Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri na Wizara husika, katika maandalizi ya kuitishwa kwa mkutano wa tabianchi unaotarajiwa kufanyika Novemba ijayo mwaka huu mjini Sharm El Sheikh, akibainisha umuhimu wa kujadili uhusiano wa mabadiliko ya tabianchi na masuala ya mwamko kwa kuzingatia maslahi ya Dunia katika mazingira, na mwelekeo wa uchumi na shughuli mbalimbali kuwa rafiki kwa mazingira, na akibainisha kuwa Misri inachukua hatua madhubuti katika suala hilo chini ya uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi.
Waziri huyo alisema: "Changamoto kubwa inayoikabili nchi ni mwamko na uelewa kuhusu masuala mengi na changamoto zinazoikabili nchi, jambo linalohitaji kila mmoja kuungana kueneza mwamko kuhusu masuala muhimu zaidi na Mabadiliko ya kisasa".
Ikumbukwe kuwa Kongamano hilo la kiutamaduni linajumuisha majadiliano na vijana kuhusu mabadiliko ya tabianchi ndani ya maandalizi ya mkutano wa kilele wa tabianchi utakaofanyika mjini Sharm el-Sheikh, na vikao vya kisanii vilivyowasilishwa na wajumbe wa Bendi ya Wizara ya Vijana na Michezo, na kuheshimu karatasi mbili bora zaidi za utafiti kwa vijana waliowasilisha kupitia kiunga cha kielektroniki cha kongamano kuhusu Mabadiliko ya tabianchi.
Comments