Katika siku yake ya pili Kikao kinachoitwa mtazamo wa vyombo vya habari wa kutatua masuala ya kiafrika, kiarabu na migogoro ya kimataifa
- 2022-03-19 11:34:06
Jumatatu,miongoni mwa shughuli za mkutano wa kwanza wa viongozi wa vijana unaotekelezwa na Wizara ya Vijana ma Michezo ikiwakilishwa katika Idara kuu ya bunge, Elimu ya uraia na Utawala mkuu wa mahusiano ya umma na vyombo vya Habari mnamo kipindi cha Machi 13 hadi 16 kwa ushiriki wa vijana na wanafunzi wa Vitivo na Sehemu za vyombo vya habari kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali vya kimisri, pamoja na washiriki 160 wanaowakilisha Vitivo na Sehemu za vyombo vya habari 36 katika mikoa yote ya Jamhuri,pamoja na Taasisi ya Tansikia ya Vijana wa Vyama na wanasiasa, ulishuhudia kikao kinachoitwa mtazamo wa vyombo vya habari wa kutatua masuala ya kiafrika, kiarabu na migogoro ya kimataifa.
Profesa. Samy Abd Elaziz, Mkuu wa zamani sana wa Kitivo cha vyombo vya habari na profesa wa vyombo ya habari vya kimataifa, alitoa mada yenye matokeo mazuri kwa wanafunzi waliohudhuria, kwa kichwa cha jinsi tunavyosimamia mgogoro?, akieleza mkakati wa usimamizi wa shida, hatari ya kudai maarifa, jinsi ya kuweka mipango ya kushughulika maoni ya umma, akiongeza jinsi ya kudhibiti migogoro katika vyombo vya habari, akizungumzia maandalizi halisi ya usimamizi wa mgogoro, kukadiria ukubwa na nguvu ya ushawishi wa vyombo vya habari, na akiongeza kuwa nchi hazijaweza kuficha au kunyamazisha migogoro, akihitimisha mazungumzo yake kuhusu ubora wa Rais Abd El Fatah El-Sisi katika kushughulika migogoro kupitia sifa tatu nazo ni: makabiliano, uwazi na utambuzi.
Ahmed Anwr, Rais wa Muungano wa Vyombo vya Habari vya Kiarabu na Wavumbuzi waarabu na Mwanachama wa Umoja wa Mataifa, alisisitizia umuhimu wa kujiandaa vyema kwa maudhui ya vyombo vya habari, inayohitaji kuharakisha kuchukua hatua,akiashiria hatua za kutengeneza programu za media katika enzi ya kasi ya habari,inayosababisha udhibiti wa haraka wa migogoro, kufafanua jukumu la vyombo vya habari kama chombo cha kuonesha mgogoro, akitumia utaratibu wa utekelezaji wa haraka, pamoja na kuonesha masuluhisho kupitia vyanzo husika.
Mbunge, Rawan Lashin, alionyesha kwamba vikundi vyote vinaathiriwa na migogoro, akionyesha umuhimu wa kujua jinsi ya kukabiliana ya migogoro, akifafanua kuwa ufahamu na maarifa ya habari na mshikamano wa serikali ndio suluhisho bora la kudhibiti shida, akisisitiza kwamba ushirikiano kati ya mashirika ya serikali unaweza kuboresha nchi na kushinda migogoro.
Ikumbukwe kwamba mihimili ya Kongamano hilo ilijumuisha vikao vingi vya mazungumzo na majadiliano, pamoja na warsha za mafunzo na kuwezesha ikiwa ni pamoja na: vyombo ya habari vya mchezo, kukataa vurugu na kutovumiliana katika viwanja vya mchezo, kupanua msingi wa mazoezi ya michezo, vyombo vya habari vya Misri, changamoto za wanawake na watoto, mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya utalii, vyombo vya habari vya ndani na kitaifa katika enzi ya Jamhuri mpya, na yanayohusu kuhimiza utafiti wa kisayansi na mawazo bunifu katika shughuli za habari? Na mtazamo wa vyombo vya habari katika kutatua masuala ya kiafrika, kiarabu na migogoro ya kimataifa na jukumu la vyombo vya habari katika kuboresha tabia za Wachipukizi na vijana,pia mikoa ya mpakani mbele ya vijana wa vyombo vya habari, na jukumu la vyombo vya habari vya kitaifa katika kukuza uelewe wa mazingira mabadiliko ya hali ya hewa , na vyombo vya habari, mabadiliko ya kidijitali na msimbo wa heshima ya Media- sheria na maadili (sera za kisasa za vyombo vya habari) pamoja na kuandaa baadhi ya ziara za ndani kwa taasisi kuu za vyombo vya habari.
Comments