Waziri wa Michezo Ampongeza Muhliba kwa Dhahabu ya Skeet katika Kombe la Dunia huko Cupros


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alimpongeza nyota wa timu ya taifa ya Upigaji Risasi Mchezaji Azmi Muhliba baada ya kupata medali ya Dhahabu katika mashindano ya Skeet kwenye michuano ya kombe la Dunia ya Upigaji Risasi ambayo shughuli zake zimehitimishwa huko Cupros hivi karibuni. 


Waziri wa Vijana na Michezo alieleza furaha yake kubwa kwa mafanikio hayo makubwa ya nyota wa timu ya taifa ya kimisri ya upigaji risasi Azmi Muhliba, akisisitiza kwamba mfumo wa upigaji risasi wa Misri kwenye kasi thabiti kuelekea kufikia mafanikio ya kimataifa kwa msaada usio na mipaka unaotolewa na Wizara ya Vijana na Michezo Shirikisho na Wachezaji.


Ikumbukwe kuwa Mpigaji Risasi Azmi Muhliba alitawazwa Oktoba iliyopita kwa medali ya shaba kwenye michuano ya kombe la Dunia huko Cupros, na mwaka jana katika michuano ya kombe la Dunia ya Upigaji Risasi,huko Italia kwenye mashindano ya Skeet alitawazwa kwa dhahabu ya Dunia.

Comments