Waziri wa Michezo azindua Kombe la Dunia la Sarakasi katika kumbi za Uwanja wa Kimataifa wa Kairo

kwa kuwepo Wakuu wa Mashirikisho mawili ya Kimataifa ya Mikono na Sarakasi



Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia ufunguzi wa Kombe la Dunia la Sarakasi la 2022 Kairo katika Mfululizo wa Mashindano ya kufikia Olimpiki ya Paris ya 2024, Mbele ya Dokta Hassan Mostafa, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono na Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Sarakasi la Kijapani Bw.Mori Watanabe, na wajumbe wa Ofisi ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa, na Meja Jenerali Khaled Shoukry, Mkuu wa Mamlaka ya Michezo ya Wanajeshi, na Dokta Ihab Amin, Mkuu wa Shirikisho la Afrika na Misri kwa Sarakasi, na Mhandisi Sherif El-Erian, Katibu Mkuu wa Kamati ya Olimpiki, Mkuu wa Muungano wa Kisasa wa Pentathlon, na wakuu wa mashirikisho ya bara.


Mwanzoni mwa hotuba yake, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alielezea furaha yake ya kukaribisha Misri  Kombe la Dunia la Sarakasi ya kiufundi kwa wanaume na wanawake, ya kufikisha Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024, Akiwasifu viongozi wa Shirikisho la Misri la Mchezo huo likiongozwa na Dokta Ihab Amin na juhudi kubwa walizozifanya mnamo kipindi cha hivi karibuni zilizojidhihirisha katika uandaaji wa michuano hiyo mikubwa ya Dunia nchini Misri.


Waziri alisema, “Nchi ya Misri iko chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi; Sasa iko tayari kuandaa hafla zote kuu za michezo baada ya miundombinu ya majengo ya michezo ikawa katika kiwango bora kulingana na mahitaji na viwango vya mashirikisho yote ya kimataifa,

Waziri huyo alimalizia hotuba yake akisema: “Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, tufungue Michuano ya Dunia ya Sarakasi ya kiufundi huko Misri."


Kwa upande wake Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, Dokta Hassan Mustafa, ameeleza kufurahishwa kwake na maendeleo makubwa yanayotokea kwa Sarakasi nchini Misri, hiyo ilikuja wakati wa sherehe za ufunguzi wa Mashindano ya Dunia ya Sarakasi ya Kiufundi kwa wanaume na wanawake, Ikizingatiwa kuwa Misri imepata hatua kubwa

kwa Sarakasi mnamo miaka iliyopita,

Hapo awali, hatukuwa na fursa za kushindana katika mashindano makubwa, na sasa Sarakasi ni miongoni mwa michezo ambayo ina uwezo mkubwa kwa mashindano ya kimataifa, Shukrani kwa uungaji mkono wa uongozi wa kisiasa nchini na juhudi na uungaji mkono wa Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy.


Mjapan, Bw. Mori Watanabe, alithibitisha kwamba anajivunia uenyeji wa Misri wa Kombe la Dunia la Sarakasi ya kiufundi kwa wanaume na wanawake, na Misri ina fahari maalum ndani ya nafsi yake, ikiashiria kwamba anafurahi sana kama anakuwepo katika nchi ya Mafarao.


Mkuu wa Shirikisho hilo alibainisha kwamba Shirikisho la Misri la Sarakasi likiongozwa na Dokta Ihab Amin, lilifanikiwa kuiweka Misri kati ya nchi kubwa katika Sarakasi ya kiufundi mnamo kipindi cha mwisho, akitoa Shukrani zake  kwa Misri ikiwakilishwa na Dokta Ashraf Sobhy Waziri wa Vijana na Michezo, aliyetoa msaada wetu mkubwa katika kipindi cha mwisho, Akiongeza kuwa tunapaswa kujivunia kile Misri iliyofanikisha katika miaka iliyopita na tuwe na miundombinu imara yenye uwezo wa kukaribisha Mashindano makubwa zaidi ya Dunia,pia Kuwepo kwa idadi kubwa ya vijana wakuu wenye uwezo wa kuandaa na kusimamia.


Mashindano hayo yanashuhudia hatua kali za tahadhari, ili kuwalinda wajumbe wanaoshiriki dhidi ya Virusi vipya vya Corona, Covid 19, kwa umuhimu wa kuzingatia maagizo ya kinga kutoka kwa Wizara ya Afya.


Kamati Kuu iandaayo Mashindano hayo ikiongozwa na Mkuu wa Shirikisho la Misri na Afrika na Mjumbe wa Ofisi ya Utendaji ya Shirikisho la Kimataifa Dk Ihab Amin, ilikuwa na nia ya kufuatilia maandalizi yote maalum ya mashindano hayo.


Misri katika ukumbi wa ndani wa Uwanja wa Kimataifa wa Kairo, inakaribisha mashindano ya Kombe la Dunia la Sarakasi la kiufundi la Wanaume na Wanawake 2022,  itakayofanyika kuanzia Machi 17-20, Pamoja na ushiriki wa washiriki 281 wanaowakilisha nchi 34, zikiongozwa na Ukraine, licha ya hali ya sasa.

Nchi hizo zilikuaj kama ifuatavyo nchi mwenyeji Misri, Albania, Algeria, Armenia, Australia, Austria, Azerbaijan, Jamhuri ya Czech, New Zealand, Ireland, Kanada, Kroatia, Kupro, Finland, Ugiriki, Hong Kong, Hungary, Iceland, Italia, Jordan. , Kazakhstan, Lithuania, Malaysia, Morocco, Norway, Poland, Afrika Kusini, Slovenia, Uturuki, Marekani, Uzbekistan, India na Qatar.


Comments