Waziri wa Michezo ashuhudia mikutano ya Shirikisho la Kamati za Kitaifa za michezo ya Olimpiki za kiafrika
- 2022-03-20 10:17:27
Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy alishuhudia matukio ya mkutano wa Shirikisho la Kamati za Michezo ya Olimpiki za kiafrika “ANOKA” unaofanyika mjini Kairo; kujadili masuala kadhaa yanayohusu mashindano ya michezo ya kiafrika yatakayofanyika mnamo kipindi kijacho.
Matukio hayo yalifunguliwa na Mustafa Braf, Mkuu wa Shirikisho la Kamati za michezo ya Olimpiki za kiafrika "ANOKA", kwa kuhudhuria Dkt. Hassan Mustafa, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, Bwana Joao kutoka Sao Tome, Makamu wa Kwanza wa Rais, Matulunga kutoka Lesotho. , Makamu wa Pili wa Rais, Vardusa kutoka Djibouti, Makamu wa Tatu, Kamal El-Helou, Makamu wa Nne, Mweka Hazina kutoka Nigeria Gomel Abu- Ahmed ,na Mhandisi Hisham Hatab, Mkuu wa Kamati ya michezo ya Olimpiki ya Misri walihudhuria mkutano huo.
Waziri huyo aliwakaribisha wageni wote nchini Misri, wawakilishi wa Shirikisho la Kamati za michezo ya Olimpiki za kiafrika "ANOKA", na kuandaa mkutano wao huko Kairo, wakati Misri inazingatia umuhimu wa kuandaa na kufanya matukio na mashindano mbalimbali ya kimataifa kutokana na nguzo kubwa zinazopatikana nchini Misri kama suala la miundombinu na uzoefu wa uandaaji wa matukio hayo.
Dkt. Ashraf Sobhy alisisitizia kuunga mkono juhudi za ANOKA, na sera yake inayolenga kuendeleza na kufufua michezo ya Afrika, na kuipandisha hadi ngazi za kwanza Duniani, pamoja na Ushirikiano na Shirikisho hilo kwa njia ya kuhimiza nafasi ya Michezo ya Misri na kuhakikisha maendeleo yanayotarajiwa katika michezo yote.
Mkuu wa Shirikisho la Kamati za Kitaifa za michezo ya Olimpiki za Kiafrika, alimtoa Dkt. Ashraf Sobhy, zawadi ya mkufu wa "ANOKA" Shukrani kwa jukumu lake wazi katika kuendeleza michezo ya Misri, na mafanikio ya uandaaji wa Misri kwa mashindano mengi ya Barani na kimataifa, pamoja na msaada wake wa kudumu kwa juhudi za Shirikisho.
Comments