Wachipukizi wa Timu ya kitaifa ya Misri washinda Algeria na kutwaa Michuano ya Afrika Kaskazini


Timu ya kitaifa ya Misri kwa Wachipukizi wazaliwao mwaka 2006, ikiongozwa na Mohamed Wahba, ilitwaa ubingwa wa Afrika Kaskazini, uliofanyika nchini Algeria, Kwa ushiriki wa timu 5, nazo ni Misri, Tunisia, Algeria, Morocco na Libya.


Katika raundi ya mwisho Misri ilishinda  Algeria kwa 1-0 katika mechi ya timu hizo mbili Jumapili, katika uwanja wa Casablanca nchini Algeria. 


Ibrahim Adel alifunga bao la ushindi kwa timu ya kitaifa  mnamo dakika ya 22; ambapo lilitengenezwa vizuri na Omar Syed Moawad, basi kuwawezesha Mafarao kuongeza alama zao hadi alama 12  kamili baada ya kushinda mechi nne walizozicheza kwenye michuano hiyo.

Comments