Waziri wa Michezo ashuhudia shughuli za Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kuogelea
- 2022-03-22 14:17:40
Dkt Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alishuhudia shughuli za mkutano wa kwanza wa kimataifa wa kuogelea, unaolenga kujadili na kushughulikia njia za kuendeleza kuogelea kwa Misri na kuifikisha viwango vya juu zaidi, kama maandalizi ya Olimpiki ya 2024, 2028.
Shughuli za mkutano huo zilihudhuriwa na Kocha Hussein Al-Musallam, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Kuogelea, Dkt Hassan Mustafa, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Mikono, Bw. Mustafa Braf, Mkuu wa Mashirika ya Olimpiki ya Afrika "ANOCA", Mhandisi Hisham Hatab, Mkuu wa Kamati ya Olimpiki ya Misri, Wissam Ram Sam, Mkuu wa Shirikisho la Afrika la Kuogelea , Mhandisi Yasser Idris, Mkuu wa Shirikisho la Misri la Kuogelea , na kundi la wakuu wa klabu, mashirikisho ya michezo na wachezaji wa Olimpiki katika kuogelea kimataifa na nchini Misri.
Katika hotuba yake, Waziri wa Vijana na Michezo alisema: “Shukrani zote kwa Shirikisho la Kuogelea la Misri kwa wazo hilo, lililotokea kwa mara ya kwanza kwa ajili ya kuendeleza mchezo wa kuogelea wa Misri, Tunathamini mahudhurio ya wachezaji wa kimataifa wa Olimpiki na wakuu wote wa klabu na Mashirikisho ya michezo na maafisa katika sekta mbalimbali za michezo, wakiongozwa na Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Kuogelea Kocha Mwanahewa.Hussein Al-Musallam na Bw. Mustafa Braf, Mkuu wa Kamati za Olimpiki za Afrika.
Waziri huyo alieleza kuwa Misri linatilia maanani kusaidia na kuendeleza kuogelea kwa Misri,kupitia kuzingatia maoni na mipango ya siku za Usoni inayokuza maendeleo ya kuogelea kama maandalizi ya Olimpiki, huko akitoa wito kwa wachezaji wa kuogelea wa Misri kufanya juhudi zaidi. kufikia ndoto kubwa zaidi, nayo ni Olimpiki 2024, 2028 na kupata matokeo na mafanikio bora zaidi katika vikao mbalimbali.sambamba na Kuunga mkono sera za Shirikisho la Kimataifa la Kuogelea, kwa Ushirikiano na Shirikisho la Kamati za Kitaifa za Olimpiki za Afrika, kuendeleza kuogelea Barani Afrika, akiashiria utayari wa Misri kukaribisha mashindano yote ya kimataifa baada ya mfululizo wa mafanikio yaliyopatikana kwa michezo ya Misri katika viwango vyote vya kimataifa na Olimpiki, chini ya uangalizi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi na msaada wake wa kudumu kwa vijana wa Misri katika nyanja mbalimbali.
Akiashiria kuwa miundombinu ya Misri katika majengo ya michezo na vijana ilianzishwa kwa kiwango cha juu zaidi kwa mujibu wa viwango vya kimataifa, hivyo kuifanya nchi ya Misri iwe maarufu zaidi na Maelekezo wa Kamati ya kimataifa ya Olimpiki, na mashirikisho ya kimataifa katika michezo mbalimbali ya watu binafsi na ya makundi kuandaa michuano ya Dunia, linaloonesha imani ya mashirikisho ya kimataifa nchini Misri na uwezo wake wa kuandaa michuano mingi ya Dunia licha ya kuenea kwa Janga la Corona.
Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Kuogelea, Kocha Hussein Al-Musallam, alielezea furaha yake akisema:
"Nina Furaha na fahari kwa niko kwenye Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, katika mkutano huu wa wakuu wa Kamati za Olimpiki, Klabu na Mashirikisho ya michezo, na serikali ya Misri ikiwakilishwa na Dkt. Ashraf Sobhy" akiongeza kuwa Misri ina miundombinu imara na ina Makada wazuri na utaalamu safi, na hilo ndilo lililoifanya iwe Mwelekezo wa Dunia ili kuandaa na kukaribisha matukio na shughuli za kimataifa za michezo.
Al-Musallam aliashiria Mwelekeo wa Shirikisho la Kimataifa la Kuogelea kueneza na kufundisha kuogelea katika nchi mbalimbali Duniani zikiwemo nchi za bara la Afrika kwa Ushirikiano na Mashirikisho ya kitaifa, ma Uanzishaji wa vituo vya kuendeleza michezo vinavyohusiana na Shirikisho la Kimataifa ndani ya nchi za Afrika kupitia itifaki za Ushirikiano na ANOKA.
Comments