Waziri wa Michezo aangalia Uwanja wa Kairo katika kujitayarisha kwa ajili ya mechi kati ya Misri na Senegal


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ameangalia Uwanja mkuu wa michezo wa kimataifa wa Kairo; kuhakikishia matayarisho yote na mipango inayohusiana na mechi  inayokusanya Misri na Senegal, Ijumaa ijayo, katika hatua ya mwisho ya kufikia Kombe la Dunia nchini Qatar.


Waziri huyo amefuatilia matayarisho yaliyofanyika ndani ya jumba kuu, Madaraja ya Uwanja, njia ya watu wa Misri kuingia kwenye mechi, hivyo hivyo matayarisho ya ardhi ya uwanja kikamilifu, na kuonekana katika sura  bora.


Dokta Ashraf Sobhy, amesisitiza ufuatiliaji wa mara kwa mara kwa mipango yote ya mechi katika viwango vya Mahali, Idara na kiufundi, kuongezeka hali ya utayari wa juu zaidi kwa mechi muhimu zijazo,akitakia bahati njema  kwa wachezaji kushinda mechi ili waweza kufikia Kombe la Dunia kabla ya mechi ya kurudi nchini Senegal.


Wakati wa Matembezi hayo Waziri wa Vijana na Michezo alikuwa pamoja na Bw.HussenMuslim Mkuu wa Shirikisho la kimataifa la Kuogelea, Bw.Mustafa Berraf, Mkuu wa Shirikisho la kamati za kitaifa za Olimpiki za Afrika "ANOCA" kando ya itifaki ya Ushirikiano iliyosainiwa kati yao, pia kwa Mahudhurio ya Jenerali Ali Darwish, Mkurugenzi Mtendaji wa Uwanja wa Kairo.

Comments