Nchi 38 zashiriki katika mkutano wa kiarabu wa kiafrika; kuimarisha jukumu la wajitolea katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya Hewa


Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza kufikia wajumbe kutoka nchi 38 kushiriki katika mkutano wa kiarabu wa kiafrika  ili kuimarisha Jukuma la Wajitolea katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, mnamo kipindi cha kuanzia (21-27) Machi hii, unaotekelezwa na Wizara kupitia Idara kuu ya Mipango ya Utamaduni na Kujitolea kwa ushirikiano na Wizara mbili za Mazingira na Rasilimali za Maji, Umoja wa Wajitolea wa Kiarabu, Kitivo cha Mafunzo ya juu na Sayansi za Mazingira katika Chuo Kikuu cha Ain Shams, Idara rasmi ya Vijana  ya Mkataba wa Mfumo wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, Wakala wa Ushirikiano wa Maendeleo wa Misri, Kituo cha Mafunzo cha Kikanda cha Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, Kitengo cha Sera na Maendeleo ya Biashara katika Ofisi ya Waziri, na Kitengo cha Hali ya Hewa katika Idara kuu ya Mahusiano ya Umma na mahusiano ya nje.


Utekelezaji wa mkutano huo unakuja ndani ya mfumo wa kuongoza Misri kwa Urais wa kikao cha ishirini na saba cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa (Sharm el-Sheikh 2022), na kwa kuzingatia matarajio ya Misiri kuendeleza yale yaliyofikiwa huko Glasgow, kuelekza ahadi katika hatua zinazoonekana, na kuendelea kuboresha juhudi za kuimarisha Kazi ya Ajenda ya Hali ya Hewa katika ngazi zote, kuamsha ushiriki wa vijana katika hafla hiyo, na vile vile kuwashughulikia vijana ya Dunia wanaangalia masuala ya hali ya hewa na kutawala ushiriki huo katika mfumo wake rasmi na wa kimataifa ufaao ili kufanikisha ukaribishaji huo wa kihistoria na kuuleta katika mfumo ufaao.


 Wajumbe kutoka Mali, Sudan Kusini, Sierra Leone, Sudan, Burundi, Mauritius, Chad, Senegal, Djibouti, Cameroon, Malawi, Gabon, Burkina Faso, Rwanda, Comoro, Bahrain, Yordani, Syria, Libya, Somalia na Yemen, Mauritania, Kuwait, Tunisia, Ufalme wa Oman, Nigeria, Iraq, Benin, Saudi Arabia, Palestina, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ghana, Liberia, Ufilipino, Finland, Lithuania, Uingereza", pamoja na ujumbe wa Misri wote watashiriki katika mkutano huo.


Mkutano huo unalenga kuunda uwezo wa vijana wa Misri kuelekea sera za hali ya hewa za ndani na kimataifa na mabadiliko ya hali ya hewa, kubadilishana mbinu bora za ushiriki wa vijana nchini Misri na katika ngazi ya kimataifa, na uwezekano wa mawasiliano, haswa katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama, kwa kuongeza kuendeleza uhusiano kati ya vijana na watoa maamuzi ili kushirikiana katika sera za hali ya hewa na mabadiliko ya hali ya hewa, kuinua sauti ya vijana wa Misri na kuingizwa kwake katika maamuzi ya ndani na ya kimataifa juu ya sera ya hali ya hewa, pamoja na maendeleo ya ushirikiano kati ya vijana wa Misri, ikiwa ni pamoja na ushiriki wa (wanawake, jamii za mitaa, vijana wanaoishi katika maeneo yenye rasilimali chache.).


Mkutano huo unalenga aina ya vijana waliojitolea ,mashirika yasiyo ya Kiserikali,  Mashirika mapya, wataalamu, mkutano unahusu mada kadhaa, ikiwa ni pamoja na "Kujitolea katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa kama chombo cha kueneza ufahamu wa masuala ya hali ya hewa, njia za kuchochea mchakato wa kujitolea katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, Jukumu la mashirika yasiyo ya kiserikali (jamii ya kiraia) katika kushughulikia masuala ya mazingira, mazoea ya ubunifu ya kuanza katika mazingira ya biashara ya hali ya hewa. Kuokoa nchi zinazoendelea zenye hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa: Jukumu la utafiti wa kisayansi katika kupata chakula na maji, kupambana na mabadiliko ya hali ya Hewa: Athari za kupanda kwa kina cha bahari katika nyanja za kijamii na kiuchumi za miji ya pwani ya Afrika, mabadiliko ya hali ya hewa na athari zake kwa Amani ya kijamii.

Comments