Waziri wa Vijana na Michezo atembelea makao makuu ya Wizara katika mji mkuu mpya wa utawala ili kufuatilia taratibu za mwisho za kupokea Waajiriwa
- 2022-03-25 19:33:49
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alitembelea makao makuu ya Wizara katika mji mkuu mpya wa kiutawala, kwa mahudhurio ya viongozi kadhaa wa Wizara, kufuatilia utayari wa makao makuu kuwapokea waajiriwa iliyopangwa kuwahamisha pale; kufanya kazi kutoka Mtaa wa kiserikali, na kuainisha hatua za mwisho za kuhamisha rasmi kwa Wizara huko mji mkuu mpya wa kiutawala.
Hiyo inatokea katika muktadha wa maandalizi ya Wizara, mashirika, na mamlaka mbalimbali nchini kuhamisha kikamilifu na kufanya kazi kutoka Mtaa wa serikali katika mji mkuu mpya wa utawala, kama utekelezaji wa maagizo ya uongozi wa kisiasa.
Waziri huyo alitembelea jengo na Ofisi mbalimbali, pamoja na kuangalia vifaa na huduma zote na vifaa vya ndani vya jengo;akisifu ubora wa vifaa hivyo vilivyozingatia utoaji wa viwango bora vya mazingira ya kazi na mtindo wa kisasa wa ujenzi.
Waziri huyo alisisitiza kuwa kuhamisha pale mji mkuu mpya wa utawala ni mabadiliko ya utawala, huduma na kiufundi ambayo hayajawahi kufanywa, pia inayochangia kuendeleza utendaji wa vifaa vya utawala vya serikali,na kuboresha huduma zinazotolewa kwa wananchi, kuboresha ubora wa maisha nchini Misri, pia ni mwanzo wa enzi mpya ya kazi ya kuboreshwa ya serikali.
Dokta Ashraf Sobhy alielekeza utoaji wa huduma zote za vifaa katika jengo, na kufanya juu chini ili kutoa vifaa vyote katika jengo hilo ili waajiriwa wa Wizara watekeleze majukumu yao kwa urahisi, akionesha umuhimu wa mabadiliko hayo katika kuendeleza na kuboresha mfumo wa kazi na ufuatiliaji katika Wizara, na kufikia utawala bora,na mabadiliko ya kidijiti katika mfumo wa kazi wa kiutawala, hilo ndilo ni lengo la Jamhuri mpya.
Comments