Wajumbe wa kiarabu na kiafrika wa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa wako katika ziara ya Chuo Kikuu cha Ain Shams, Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Tafiti za Mazingira
- 2022-03-25 19:44:41
Wizara ya Vijana na Michezo kuliandaa ziara ya Chuo Kikuu cha Ain Shams, Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Tafiti za Mazingira kwa ajili ya wajumbe wa kiarabu na kiafrika walioshiriki katika mkutano wa kiarabu na kiafrika; kuimarisha jukumu la wajitolea katika makabiliano ya mabadiliko ya hali ya hewa, inayotekelezwa na Wizara kupitia ya Idara kuu kwa programu za kiutamaduni na za kujitolea kwa ushirikiano na Wizara ya Mazingira na Wizara ya Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, Shirikisho la Kujitolea la Kiarabu, Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Sayansi ya Mazingira, Chuo Kikuu cha Ain Shams, Idara rasmi ya Vijana na Wachipukizi kwa mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa na wakala ya Ushirikiano wa kimisri kwa ajili ya Maendeleo, Kituo cha Mafunzo cha kikanda cha Rasilimali za Maji na Umwagiliaji, Kitengo cha Sera na Maendeleo ya Biashara katika Ofisi ya Waziri, na Kitengo cha Hali ya Hewa katika Idara kuu kwa Mahusiano ya Umma na Nje mnamo kipindi cha kuanzia 21 hadi 27 Machi hii.
Wajumbe walioshiriki katika ziara hiyo waliambatana na Mkurugenzi Mkuu wa Utawala wa Programu za Hiari na Skauti, Jihan Hanafi, Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Jumuiya ya Kujitolea ya Kiarabu, Dkt Khaled Al-Azab na walipokelewa na Dkt. Noha Samir Donia, Mkuu wa Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Tafiti za Mazingira katika Chuo Kikuu cha Ain Shams. Na kikundi cha wanachuoni wa Kitivo, kwa Utaratibu wa Dkt. Mohamed Shaheen, Mratibu wa Tume ya kufikia Cop.
mkutano huo unahudhuriwa na wajumbe kutoka nchi 38, zikiwemo Kenya, Mali, Sudan Kusini, Sierra Leone, Sudan, Burundi, Mauritius, Chad, Senegal, Djibouti, Cameroon, Malawi, Gabon, Burkina Faso, Rwanda, Comoro, Bahrain, Jordan. , Syria, Libya, Somalia, Yemen, Mauritania, Kuwait, Tunisia, Ufalme wa Oman, Nigeria, Iraq, Benin, Saudi Arabia, Palestine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ghana, Liberia, Ufilipino, Finland, Lithuania, Uingereza, pamoja na ujumbe wa kimisri.
Wakati wa ziara yao kwa Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Tafiti za mazingira cha Chuo Kikuu cha Ain Shams, Wajumbe hao walijua mada kuu, idara za kisayansi, vituo vya huduma na Tafiti Kitivoni, kikao kiliandaliwa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na vipimo vilivyoandamana vya Nishati mbadala, mifumo ya kuchakata takataka, mifumo bunifu ya kilimo na vitengo mbalimbali vya uzalishaji.
Baada ya hapo, washiriki walielekea kwenye Kitengo cha Mabadiliko ya Kijani, wakafahamu na vituo na vitengo vya uzalishaji katika kitengo hicho, kisha wakafahamu kitengo cha kuchakata takataka za karatasi na utengenezaji wa karatasi zilizosindika, kisha ziara kwa kitengo cha kutenganisha takataka ngumu na kukandamiza.
Baada ya hapo kikao kiliandaliwa na kusimamiwa na Dkt.Ahmed Al-Awadi kutoka Idara ya Uhandisi wa Mazingira Kitivoni hapo, ambapo alizungumzia vyanzo vya Nishati mbadala, vyanzo vya Nishati ya Jua, seli za Jua na muundo wake, na jinsi ya kupata Nishati safi,pia kupunguza uzalishaji kutoka kwa vyanzo vya Nishati. .Pia, kikao kingine kiliandaliwa kuhusu kalori, Nishati na kifungu cha Nishati kutoka kwa Mzalishaji hadi kwa Mtumiaji, inayoitwa Idara ya Nishati, na mhadhara wa kuchakata takataka ngumu na utengenezaji wa msingi uliochakatwa.
Baada ya kumaliza vikao hivyo, wajumbe wa nchi za Kiarabu na kiafrika walishiriki kupanda miti kadhaa katika eneo la upandaji miti la Kitivo hicho, na kuweka bendera za nchi karibu na miti hiyo, kama msisitizo wa kushirikiana na mshikamano kati ya watu katika kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.
Mwishoni wa ziara hiyo, ndani ya Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Tafiti za Mazingira, vyeti viligawanyika kwa washiriki kama Mabalozi wa hali ya hewa ya kiarabu na kiafrika.
Comments