Waziri wa Vijana na Michezo azindua Mkutano wa Kiarabu wa Kiafrika kwa Kuimarisha Jukumu la Wajitolea Katika kupambana na Mabadiliko ya hali ya hewa


Jumanne , Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Mkuu wa Ofisi ya Utendaji ya Baraza la Mawaziri wa Vijana na Michezo wa Kiarabu, alizindua shughuli za mkutano wa kiarabu wa kiafrika ili kuimarisha jukumu la wajitolea  katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa .unaotekelezwa na Wizara kupitia Idara kuu ya Programu za Utamaduni na Kujitolea kwa kushirikiana na Wizara mbili za Mazingira, na Rasilimali za Maji na Umwagiliaji mnamo kipindi cha Machi hii 21-27.


Katika hotuba yake Waziri wa Vijana na Michezo alieleza kuwa Dunia imeanza kushuhudia mabadiliko mengi yanayoonekana kutokana na matukio ya haraka mfululizo yakiwemo mabadiliko ya hali ya hewa na kuna changamoto kubwa za kiuchumi na hali ya hewa zinazoikabili Dunia. 


Dkt. Ashraf Sobhy alisema: “Sisi nchini Misri tumewaweka vijana wetu katika kipaumbele cha makundi yanayopata uangalizi na matunzo kwa mustakabali usio na migogoro, na tumefanikiwa kutengeneza nafasi ya pamoja ambapo tunakutana na kudhibiti tofauti zetu vizuri sana. na Mikutano ya kitaifa ya vijana imefanikiwa kufikia hali ya kipekee ya mazungumzo, kupitia Jukwaa la Vijana Duniani, ambao umekuwa jukwaa la mazungumzo kati ya vijana Duniani kwa Ufadhili na heshima ya Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri". 


Waziri huyo aliongeza: “Leo tunazindua mkutano wa kiarabu wa kiafrika ili kuimarisha jukumu la wajitolea katika kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa, Ambapo vijana kutoka kwa wana wa nchi zetu za Kiarabu na Bara la Afrika lenye matumaini watakutana nchini Misri ili kubadilishana maoni na kuangalia mustakabali ukiwa na Amani na Upendo.



Alieleza kuwa Ukaribishaji wa Misri wa Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa Cop27 huko Sharm El-Sheikh ni kama mwakilishi wa bara la Afrika na Ulimwengu wa Kiarabu,  inayotulazimisha kufanya kazi ili kufikisha sauti ya vijana wa maeneo hayo mawili Duniani, na kuonyesha kiwango cha uharibifu uliosababishwa kwao kama matokeo ya moja kwa moja ya viwango vya juu vya gesi chafu kwenye angahewa, akionesha kuwa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, anatoa umuhimu mkubwa kwa faili hilo. 


Dkt. Ashraf Sobhy aliendelea, "Leo tunakutana ili kushauriana na kujadiliana taratibu na jinsi ya kuunga mkono juhudi za vijana wanaojitolea Duniani kote kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa, na hatua muhimu za  kuishi na athari za hali ya hewa. 


Sherehe ya ufunguzi ilihudhuriwa na Hassan Bou Hazaa, Mwenykiti wa Shirikisho la kiarabu la Kujitolea , Dkt Mamdouh Rashwan, Katibu Mkuu wa Shirikisho la kiarabu la Vijana na Mazingira , na wawakilishi wa Taasisi zishirikizo katika kuandaa mkutano huo, na Dkt Maged El Azazi, Mwenykiti wa Shirikisho la Vituo vya Vijana vya Misri, na kutoka Wizara ya Vijana na Michezo, Meja Jenerali Ismail El Far, Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara hiyo, Dkt, Abdullah Al-Batish, Msaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo, Bi.Najwa Salah, Mkuu wa Idara kuu ya Programu za Utamaduni na Kujitolea, Ahmed Afifi, Mkuu wa Idara Kuu na Elimu ya Uraia ya Bunge, Manal Gamal, Mkuu wa Idara kuu ya Miradi na Mafunzo ya Vijana, Dk Mervat Sayed Ahmed, Mkuu wa Idara kuu ya Miji ya Vijana, na Alaa El-Desouky, Mkurugenzi Mkuu wa programu za kisanaa na kiutamaduni, Bi.Jihan Hanafi, Mkurugenzi Mkuu wa programu za kujitolea na skauti, na  Bw.Reda Saleh Taha, Mkurugenzi Mkuu wa mahusiano ya umma na nje.


Mkutano huo unaandaliwa na Shirikisho la kiarabu la kujitolea, Kitivo cha Mafunzo ya Juu na Sayansi za Mazingira katika Chuo Kikuu cha Ain Shams, Idara Rasmi ya Vijana na Mkataba wa Mfumo wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya hali ya hewa, Na Wakala ya Misri ya Ushirikiano kwa ajili ya maendeleo, Kituo cha Mafunzo cha Kikanda cha Rasilimali za Maji na Umwagiliaji Kitengo cha Sera na Maendeleo ya Biashara katika Ofisi ya Waziri, na Kitengo cha Hali ya Hewa katika Idara kuu ya Mahusiano ya Umma na Nje. 


Mapema, Wizara ya Vijana na Michezo ilitangaza ushiriki wa wajumbe kutoka nchi 38 katika mkutano huo zikiwemo nchi za “Kenya, Mali, Sudan Kusini, Sierra Leone, Sudan, Burundi, Mauritius, Chad, Senegal, Djibouti, Cameroon, Malawi, Gabon, Burkina Faso, Rwanda, na visiwa.” Comoro, Bahrain, Jordan, Syria, Libya, Somalia, Yemen, Mauritania, Kuwait, Tunisia, Oman, Nigeria, Iraq, Benin, Saudi Arabia, Palestine, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Ghana, Liberia, Ufilipino, Finland, Lithuania, Uingereza", pamoja na ujumbe wa Misri. 

Comments