Vijana na Michezo: Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wazindua Fomu ya Ushiriki kwa kundi la tatu
- 2022-03-29 12:30:19
Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dokta.Ashraf Sobhy, ilitangaza uzinduzi wa Fomu ya kujiandikisha katika kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, chini ya kauli mbiu ya “Ushirikiano wa Kusini- Kusini na Vijana wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote chini ya Ufadhili wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, unaopangwa kufanyika mnamo Juni ijayo.
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kuwa Wizara inatekeleza mipango, mikutano, programu, shughuli na matukio mengi yenye lengo la kuimarisha Ushirikiano na mawasiliano kati ya ndugu wa Afrika na kufanya juu chini kwa kuimarisha uwanja wa uwezeshaji wa vijana na kuendeleza uwezo wao katika uongozi na kuchukua maamuzi na kufanya kazi ili kuwekeza nguvu za vijana waafrika.
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, unalenga kuangazia jukumu la Vijana wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote katika kukuza Ushirikiano wa Kusini-Kusini kwa kuzingatia Ulimwengu unaobadilika haraka na jinsi ya kukuza Ushirikiano huo kupitia Vijana kama Utaratibu muhimu na endelevu, pamoja na kutilia mkazo nafasi ya wanawake, kwa hivyo, kauli mbiu ya Udhamini mwaka huu iwe na “Ushirikiano wa Kusini- Kusini na Vijana Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote.
Unalenga vijana na wasichana wa Nchi za harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki ambao ni watoa maamuzi katika sekta ya umma, wahitimu wa programu ya Kujitolea wa Umoja wa Afrika, viongozi watekelezaji katika sekta binafsi, wawakilishi wa matawi ya kitaifa ya vijana wa harakati ya kutofungamana kwa upande wowote , wanaharakati wa mashirika ya kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa ya vijana, wajumbe wa mabaraza ya kienyeji, viongozi vijana wa vyama Maprofesa wa Vyuo Vikuu, watafiti katika vituo vya utafiti wa kimkakati na mawazo, wanachama wa mashirika ya kitaaluma, Watangazaji na Waandishi wa Habari, wajasiriamali wa kijamii na wengine.
** Wale wanaotaka kushiriki na kujua maelezo zaidi, wanaweza kupeleka maombi na kujaza Fomu hiyo kupitia kiungo kifuatacho:-
Comments