Vijana na Michezo yatangaza kuanza maandalizi ya Kongamano la Vijana la Hali ya Hewa la COY17 na uhamisho wake kutoka Uingereza hadi Misri
- 2022-03-30 15:42:57
Sobhy: Kongamano la Vijana la Hali ya Hewa la COY17 ni fursa mpya kwa Mkutano wa Vijana wa Dunia nchini Misri
Wizara ya Vijana na Michezo kwa kushirikiana na Wizara ya Mazingira na kwa uratibu na Wizara ya Mambo ya Nje, ilitangaza kuhamisha Kongamano la Vijana la Hali ya Hewa la COY17 kwenda Misri, linalofanyika kando ya Mkutano wa Kilele cha Nchi Wanachama za Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi COP27, ambalo Misri itakuwa mwenyeji wake mwaka huu huko Sharm El-Sheikh.
Hafla ya tangazo hilo imekuja mbele ya Waziri wa Vijana na Michezo Dk Ashraf Sobhy wakati wa kufunga Kongamano la Waarabu na Waafrika la Kuimarisha Nafasi ya Wajitolea lililotekelezwa na Wizara ya Vijana kwa kushirikisha Nchi 38 za Kiarabu na Kiafrika na ushiriki wa heshima wa Asia na Ulaya, na mahudhurio ya Bi. Elena Banova, Mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Misri,Bw. Zan Northcott, Mratibu wa Idara Rasmi ya Vijana na Wachipukizi wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, na Bw. Jan Carrell, Mratibu wa Kongamano la Vijana la COY16, lililofanyikwa huko Glasgow, na Mhandisi.Abdullah Imad, Mratibu wa Kitaifa wa Kongamano la Vijana la COY17.
Dkt Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza kwamba lengo la Mkutano wa Vijana wa Hali ya Hewa wa COY ni kuwawezesha Vijana na kuleta rasmi sauti zao katika mchakato wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kuunda sera kati ya serikali za mabadiliko ya tabianchi. akibainisha kuwa Kongamano la Vijana wa Hali ya Hewa la COY linafanyika katika mji huo huo wa kufanyika Mkutano wa Vyama hivyo ukitanguliwa kwa siku kadhaa pamoja na waraka inayowakilisha sauti ya Vijana Duniani inatoka humo, inqwasilishwa mkutano wa vyama COP, akisisitiza haja ya kujiandaa vyema kwa hilo kwa njia ya mafunzo na kuongeza uelewa miongoni mwa Vijana katika uwanja wa mabadiliko ya hali ya hewa katika ngazi ya kijamii.
Waziri huyo aliashiria kuwa Kongamano la Vijana la Hali ya Hewa la COY17 ni fursa mpya kwa vijana Duniani kukutana nchini Misri baada ya Kongamano la Vijana Duniani, linalothibitisha kuwa Misri ni mahali pa mikutano ya Vijana kutoka pande zote za Dunia. .
Kwa upande wake Bw.Zan Northcott alisema: “Nimefurahishwa sana na kile nilichokishuhudia Misri katika suala la uwezeshaji wa kweli wa Vijana, na imani ya uongozi wa kisiasa nchini kwa viongozi vijana, pia. kama ukaribishaji mzuri na mpangilio mzuri, pamoja na shauku kubwa ambayo uongozi wa kisiasa wa Misri unashikilia kwa kuandaa mkutano wa hali ya hewa utakaoandaliwa huko Sharm El-Sheikh Novemba ijayo, inayoonesha ufahamu wa kweli wa uzito wa hali ya hewa, na ufahamu kamili wa umuhimu wa hatua za pamoja za kimataifa.
Ikumbukwe kuwa Kongamano la Vijana wa Hali ya Hewa wa COY ni kongamano rasmi la vijana lililopitishwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, unaofanyika kwa kushirikisha washiriki karibu 2,000 Duniani kote, pembezoni mwa Mkutano wa kilele wa Nchi Wanachama wa COP, unaokaribishwa huko Sharm el-Sheikh mwaka huu.
Comments