Waziri wa Michezo akutana na Mkuu wa FIFA, Gianni Infantino pembezoni mwa mkutano wa Kilele cha Serikali huko Dubai
- 2022-04-01 15:58:41
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na Bw. Gianni Infantino, Mkuu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa na Mheshimiwa Sheikh Rashid El Nuaimi, Mkuu wa Chama cha Soka cha Emirats, Mkuu wa Idara ya Manispaa na Mpingo mjini Ajman, Makamu wa Mkuu wa Kitu cha Vijana wa Kiarabu, kando ya mkutano wa Kilele cha juu cha serikali za Dunia huko Dubai, UAE
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Bw. Gianni Infantino, Mkuu wa Shirikisho la Soka la kimataifa pamoja na Mheshimiwa Sheikh Rashid El Nuaimi, Mkuu wa Shirikisho la Chama cha Soka cha Emirats na Mkuu wa Idara ya Manispaa na Mpango mjini Ajman, na Makamu wa Mkuu wa Kitu cha Vijana wa Kiarabu walitembelea kuona makao makuu ya mkutano wa Kilele cha juu cha Serikali za Dunia 2022, inayozinduliwa kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Sheikh Mohamed Bin Rashid Al maktuom, Makamu wa Mkuu wa Jimbo hilo, Waziri Mkuu na mtawala wa Dubai, katika mkusanyiko mkubwa wa serikali wa kipekee Duniani, kutabiri mustakabali wa ulimwengu kwa ushiriki wa viongozi, Mawaziri Wakuu, maafisi wakuu wa kimataifa, Wafikiri na Wataalamu.
Mkutano huo utawasilisha, vikao vikuu zaidi ya 100, vya majingiliano na mazungumzo ya changamoto kuu za ulimwengu za sasa na zijazo, njia za kuboresha utendaji wa serikali, kuimarisha uwezo wa serikali kutarajia na kujiandaa kwa mabadiliko ya haraka na kubuni Masuluhisho yanayohakikisha kuitumia katika kuboresha maisha ya jamii, pia inaagazia matatajio ya maendeleo yajayo katika sekta mablimbali za Sayansi, Teknolojia, Matibabu na kijamii, na jinsi ya kuwekeza na kuielekeza kwa maslahi ya jamii na kuhakikisha ujenzi wa mustakabali endelevu kwa vizazi vijavyo.
Mkutano wa kilele cha Serikali za Dunia 2022 ulishuhudia ushiriki mpana wa zaidi ya watu 4000 kutoka nchi 190, pia katika vikao vyake na mazungumzo yake hushiriki jopo la wasemaji wasomi,likiwa pamoja na maafisa mashuhuri zaidi wa serikali, Wakuu wa Taasisi, Mashirika ya kimataifa, Wakuu wa Kampuni za kimataifa, Wajasiriamali maarufu katika sekta ya kibinafsi Duniani.
Comments