Waziri wa Vijana na Michezo atia saini itifaki ya Ushirikiano na mwenzake wa Angola



Jumatano, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, ametia saini itifaki ya Ushirikiano na Bi. Ana Paula, Waziri wa Vijana na Michezo wa Angola, na Bw. Titi Antonio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Angola; kuimarisha Ushirikiano wa pande mbili mnamo kipindi kijacho katika nyanja za Vijana na Michezo.

Hafla za utiaji saini huo zilihudhuriwa na Balozi Nelson Manuel, Balozi wa Angola mjini Kairo, na idadi ya wawakilishi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri.

Itifaki hiyo inajumuisha Ushirikiano katika uwanja wa Vijana, Kwa upande wa kushiriki katika kambi za vijana na za kujitolea, kubadilishana uzoefu katika uwanja wa Teknolojia, uongozi wa vijana, na Ujasiriamali, na kukuza na kuhimiza mijadala inayohusiana na utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu, na kutekeleza programu za kubadilishana Vijana.

Katika kiwango cha Michezo, itifaki inalenga kuimarisha ubadilishaji wa shughuli za michezo na kusaidia kubadilishana katika maeneo ya mafunzo, ukuzaji wa mitaala na usimamizi wa michezo, Pamoja na Ushirikiano katika uwanja wa tiba ya michezo, kuhimiza na kusaidia ubadilishaji wa teknolojia na habari, programu za maendeleo ya Tafiti katika uwanja wa Michezo, na ushiriki katika mikutano, kozi za mafunzo na mazoezi kwa makocha na Refa, yanayofanyika katika nchi hizo mbili. 

Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kina ya mahusiano yaliyopo pamoja na Angola, Na kutafutia kuimarisha viungo vya Ushirikiano wa pamoja katika nyanja mbalimbali mnamo kipindi kijacho kwa kuzingatia maagizo ya uongozi wa kisiasa katika kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia na nchi mbalimbali ndugu za Kiafrika.

Waziri huyo amekaribisha uwepo wa ujumbe wa ngazi ya juu kutoka Nchi ya Angola   unaotembelea Misri sasa,na alianza mazungumzo yake kwa kukutana na Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri kwa ajili ya kujadili njia za kuchanganya juhudi na kuimarisha Ushirikiano kati ya pande za Misri na Angola.

Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo wa Angola alisifu Ushirikiano wa manufaa na Misri kwa kuzingatia umakini wa uongozi wa kisiasa wa Angola katika kukuza mahusiano ya nchi mbili, na Ushirikiano wa pamoja kati ya nchi hizo mbili katika nyanja mbalimbali, zikiwemo za Vijana na Michezo.

Comments