Dkt.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, amefanya mkutano pamoja na Kamati iandaayo mikutano ya Shirika la Kupambana na Madawa ya Vichocheo Duniani (WADA) inayoongozwa na Dkt.Hazem Khamis, Mkuu wa Shirika la Kupambana na Madawa ya Vichocheo nchini Misri "NADO", kujadili maandalizi ya Misri kuhusu kukaribisha kwa mikutano ya Shirika hilo Mei ijayo, itakayokaribishwa kwa mara ya kwanza nchini Misri na ya pili Barani Afrika.
Mkutano huo ulijadili Kuonesha mahitaji ya Shirika la Dunia la Kupambana na Madawa ya Vichocheo, yanayojumuisha Miundombinu ya teknolojia ya habari, maandalizi mazuri ya kilojistiki na taratibu zinazohusiana na kuandaa matukio ya Ofisi ya kiutendaji na mkutano wa baraza la Idara, pamoja na kuzungumzia malazi yatakayotolewa kwa washiriki wa mikutano.
Waziri wa Vijana na Michezo alithibitisha nia ya kuunga mkono juhudi za Shirika la Dunia la Kupambana na Madawa ya Vichocheo, na kueneza ufahamu wa hatari ya kutumia Vichocheo hivyo kwa wanariadha, akisisitizia umuhimu wa kutoa uwezekano wote ili kufanikisha tukio hilo na kulionekana kwa sura inayofaa nafasi ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, katika kuandaa matukio na mashindano mbalimbali ya kimataifa, kwa kuzingatia kwa imani ambayo Misri inayo na Mashirikisho ya Michezo kwa uwezo wake wa kupanga.
Comments