Waziri wa Vijana na Michezo ashuhudia ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Kikapu Afrika BAL


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Dokta Magdy Abu Farikha, Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri, walishuhudia ufunguzi wa Michuano ya Mpira wa Kikapu ya Afrika ya BAL, kwa mahudhurio ya Amadou Gallo Vall, Mkuu wa Shirikisho la Mpira la Kikapu Afrika (BAL), Victor Williams, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Mpira wa Kikapu Afrika, Edekembo Mutombo ni Balozi wa NBA wa mashindano hayo yanayofanyika katika mkusanyiko wa kumbi za Dokta Hassan Mustafa kuanzia Aprili huu tarehe 9 hadi 19.

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alielezea kukaribisha Misri kwa Michuano hiyo katika toleo lake la pili, baada ya kufanyika toleo la kwanza nchini Rwanda.

Akisisitiza kwamba Misri ikawa ina Miundombinu imara na Rasiliamali za watu zilizofunzwa na wenye sifa kwa ajili ya Kuandaa mashindano makali na makubwa zaidi ya kimataifa na Duniani.

Waziri huyo alihitimisha hotuba yake akitakia kila la heri kwa timu zote zinazoshiriki mashindano hayo.
Wakati Amadou Gallo Val, Mkuu wa Mashindano ya Afrika kwa Klabu BAL, alionesha furaha yake ya mpangilio mzuri wa mashindano hayo na Misri, Akisisitiza kuwa hali ina shauku kubwa na itahimizwa wachezaji kushiriki mashindano hayo.


Shughuli za Kundi la Nile huanza katika Mashindano ya Afrika kwa Klabu kwa Mpira wa Kikapu  BAL, pamoja na ushiriki wa Zamalek, " Yenye Lakabu", Ambayo ni pamoja na: Zamalek ya Misri, Cobra Sport ya Sudan Kusini, Petro de Luanda ya Angola, Fab ya Cameroon, Espoir ya Congo, Cape Town Tigers ya Afrika Kusini.

Na klabu ya Zamalek ilifungua duru yake katika mashindano hayo Mbele ya Cobra Sport, bingwa wa Sudan Kusini, klabu ya Zamalek ilishinda 80-63.

Imepangwa katika mechi yake ya pili, Zamalek itakabiliana na Cape Town Tigers ya Afrika Kusini, Jumanne ijayo.

Comments