Waziri wa Vijana na Michezo akutana na wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa kujadili faili kadhaa za ushirikiano wa pamoja


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, katika maandalizi ya Misri kwa kuupokea Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa COP27, na kujadili masuala ya vijana kuhusiana na masuala ya hali ya hewa na kuratibu ushirikiano wa pamoja katika faili muhimu katika maeneo ya ushirikiano wa pamoja, Kwa mahudhurio ya Balozi Alina Panova, Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Misri, Eric Ochlan, Mkurugenzi wa ofisi ya ILO nchini Misri,na Jeremy Hopkins, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto “UNICEF”, na Frederica Meyer, mwakilishi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa kwa Idadi ya Watu nchini Misri, na kundi la viongozi wa Wizara.


Mkutano huo ulishughulikia fursa za ushirikiano wa pamoja katika maandalizi ya Mkutano wa Hali ya Hewa, COP27, na uanzishaji wa Mkutano wa Vijana wa Hali ya Hewa COY, ambao ni mkutano rasmi wa vijana uliopitishwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi, unaofanyika kwa kushirikisha karibu washiriki 2,000 kutoka Duniani kote, Pembezoni mwa mkutano wa kilele wa nchi wanachama wa COP, utakaofanyika huko Sharm El-Sheikh mwaka huu, kama Mkutano huo uligusia nukta ya ngazi ya juu wa kikanda kuhusu mafunzo ya vijana, ujuzi, ushirikishaji wa kijamii, na mpito wa kazi nzuri utafanyika Mei ijayo katika mji mkuu wa Jordani, Amman, ikiandaliwa na ofisi ya kanda ya Umoja wa Mataifa.


Mkutano huo pia uligusia maandalizi ya kisasa ya uzinduzi wa Mkakati wa Kitaifa wa Vijana wa Misri wa 2022-2027, ambao Wizara ya Vijana na Michezo iliutayarisha kwa ushirikiano na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu na Chuo cha Kiarabu cha Sayansi, Teknolojia na Usafiri wa Bahari, Ilikubaliwa kufanya mkutano na maafisa wa programu za Umoja wa Mataifa nchini Misri na vikundi vya kiufundi ili kujadili uchunguzi au marekebisho yoyote na kujadili fursa za ushirikiano katika faili hiyo.


Kwa upande wake Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alithibitisha kuwa Wizara ya Vijana inashuhudia mafanikio makubwa katika nyanja za ukarabati wa vijana kwa soko la ajira na ujuzi wa kidigitali kupitia Jukwaa la Ajira la Misri, jukwaa la TAWAR na mengine,akibainisha kuwa vijana wamekuwa na sehemu kubwa ya uungaji mkono na matunzo ya Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi tangu dakika za kwanza za kushika madaraka kwa nchi, na daima amekuwa akiwaweka mbele katika safu na masuala, mahitaji yao yameongoza ajenda ya hatua ya kitaifa. Shukrani kwa ufadhili na usaidizi huo, wamekuwa mojawapo ya shabaha muhimu zaidi za mipango ya kina ya maendeleo ambapo Misri inashuhudia kwa sasa.


Kwa upande wao, wawakilishi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Misri wamepongeza juhudi zinazofanywa na Wizara ya Vijana na Michezo katika faili ya ukarabati wa vijana kwa soko la ajira na kuboresha ujuzi wao, huku wizara hiyo ikifanya kazi kwa mashirikiano mengi ili kufikia Upeo wa faida kwa idadi kubwa ya vijana, na furaha yao katika kukaribishwa kwa Waziri kufanya kazi ya kuandaa dhamira ya kitaifa itakayozinduliwa Wakati wa mkutano wa Jordani, kuhakikisha uwakilishi wa kitaifa unaojumuisha ushiriki hai wa taasisi na mashirika ya kijamii.


Pande hizo mbili zilikubaliana kwa haja ya kutafuta kufikia sera inayozingatia ajira, mipango na utawala, pamoja na kuhakikisha kwamba vijana wanapata ujuzi wa kimsingi na wa kidijitali, kujiandaa kwa taaluma na ujuzi wa siku zijazo, na kuunda na kupanua kazi na kujitegemea fursa za ajira kwa vijana، Mikutano kadhaa iliyofuata ya vikundi vya pamoja vya kiufundi ilifanyika ili kuamsha matokeo ya mkutano na kujadili na kukuza fursa za ushirikiano wa pamoja katika kutafuta ushirikiano na kwa kuzingatia malengo ya Maendeleo Endelevu.

Comments