Kwa mara ya kwanza, Misri yaandaa Kongamano la Kimataifa (Usalama na Amani katika Soka Barani Afrika)

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF),Veron Mosengo-Omba,Kwa mahudhurio ya Rais wa Shirikisho la Soka la Misri, Gamal Allam,  kuhusu mjadala wa kukaribisha Misri kwa  Kongamano la kimataifa lialoitwa (Usalama na Amani katika Soka Barani Afrika).


Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy,  alisifu uungaji mkono wa Shirikisho la Afrika kwa Misri kufanya Kongamano la Kimataifa la Usalama na Amani katika Soka Barani Afrika, akieleza kuwa Misri limekuwa na uzoefu mkubwa katika fani ya uchezaji wa mechi mbalimbali na utaratibu wa kuandaa kuingia na kutoka kwa mashabiki, pamoja na suala la Usalama.


Waziri huyo alisisitiza kwa Katibu Mkuu kwamba Misri ina nia ya kutoa aina zote za msaada na huduma kwa maendeleo ya mfumo wa Soka wa Afrika ili kuuweka katika hadhi yake ya kimataifa, Kwa kuzingatia maendeleo makubwa yanayoshuhudiwa na Miundombinu ya michezo ya Misri na uwezo wa kiutawala, kiufundi,  vifaa ' logistics ' na watu pia za Misri.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa CAF alitoa Shukrani zake na kupongeza juhudi za serikali na msaada wake endelevu kwa mfumo wa Soka wa Afrika, akibainisha kuwa kipindi kijacho kitashuhudia mambo mengi ya ushirikiano katika nyanja nyingi.


Veron alieleza furaha yake kwa Misri kulikaribisha Kongamano la Kimataifa la Usalama na Amani katika Soka Barani Afrika, akisisitiza kuwa Idara ya Usalama na Amani ya Shirikisho la Afrika iligundua kuwa Misri ni mfano wa kuigwa na nchi zote za Afrika.


Ambapo imepangwa kuwa Waziri na taifa la Misri watawasilisha uzoefu wa mafanikio yao katika kuandaa mashindano na matukio mbalimbali ya michezo.


Kikao hicho kilijumuisha kujadili masuala mengi ya ushirikiano pamoja na Shirikisho la Soka la Afrika, ambacho ni pamoja na taratibu za kuanzisha kiwanja cha michezo cha Shirikisho la Soka la Afrika kwenye eneo kubwa inatolewa kupitia mamlaka za serikali zinazohusika, na hivyo ni kutokana na udhibiti uliojumuishwa katika mkataba wa makao makuu ya CAF,  ulioidhinishwa mnamo 2019.

Comments