Waziri wa Michezo asaini itifaki ya Ushirikiano kati ya Wizara na NBA Afrika, kwa mahudhurio ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri

Na kufungua kwa uwanja wa mpira wa kikapu katika Klabu ya Tersana

Kwa kuzingatia mpango wa Wizara ya Vijana na Michezo wa kuendeleza mfumo wa mpira wa kikapu wa Misri Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, alitia saini hati ya maelewano na Ushirikiano wa pamoja kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na NBA Afrika, Jumapili katika makao makuu ya Wizara, Kwa mahudhurio ya Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri, linalojumuisha kuimarisha Ushirikiano katika kukuza elimu ya mpira wa kikapu kati ya Vijana wa Misri katika ngazi ya chini na kuongeza ushiriki kati ya vijana na wasichana nchini Misri, pamoja na kuongeza maendeleo ya vipaji vya wasomi wa mpira wa kikapu nchini Misri.

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliwakaribisha waliohudhuria katika nchi yao ya pili, Misri, akieleza kuwa Wizara inaratibu na Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri kuendeleza mpira wa kikapu na kupanua msingi wa mazoezi kati ya Vijana.

Sobhy katika hotuba yake, aliashiria kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ina programu nyingi za kugundua watu wenye vipaji na kuwagundua tangu wakiwa wadogo na kuendeleza vipaji hivyo ili kusaidia timu ya kitaifa.

Aliongeza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo inapenda kushirikiana na NBA Afrika kukuza mpira wa kikapu nchini Misri kwa kutekeleza programu kadhaa za NBA Afrika. Na hiyo kupitia uzinduzi wa kozi za mafunzo na ligi za NBA kwa Wachipukizi na Vijana nchini Misri na kufanya warsha za elimu ya mpira wa kikapu na warsha ya makocha wa kitaifa na waelimishaji, na kutekeleza programu za kukuza vipaji vya wasomi wa Misri katika mpira wa kikapu.

Akieleza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo kupitia Ushirikiano huo itaratibu na Wizara ya Elimu katika shule na nyingine..

Kwa upande mwingine, Waziri huyo,Dokta Ashraf Sobhy, na Mkuu wa Chama cha Afrika BAL, "Bwana Amadou Gallo", na Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri, Dokta Magdy Abu Farikha, walifungua uwanja wa mpira wa vikapu katika Klabu ya Tersana baada ya kuendelezwa na kuanzishwa na Chama cha Mpira wa Kikapu cha Afrika BAL.

Huku Mkuu wa Chama cha African Association BAL,"Amadou Gallo", akijieleza furaha yake kwa kushirikiana na Misri na Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy na kusisitiza kuwa Jumuiya ya Afrika inalenga kujenga viwanja na kumbi za mpira wa kikapu salama,lililowafanya kuanza kujenga na kuendeleza uwanja wa mpira wa kikapu katika Klabu ya Al-Tersana.

 Wakati Mkurugenzi Mtendaji wa Jumuiya ya Afrika, "Victor Williams", alisisitiza kuwa Misri ina utamaduni na utaalamu mkubwa katika mpira wa kikapu, na mnamo siku chache zilizopita imeshuhudia kiwango cha upendo wa watu wa Misri kwa mpira wa kikapu.

Akibainisha kuwa alihisi maelewano makubwa kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Misri katika kueneza mpira wa kikapu.

Alisema: "Maelewano hayo yalitufikisha katika hali tuliyo sasa, ambayo ni ufunguzi wa uwanja wa mpira wa kikapu katika Klabu ya Tersana, ambayo ni biashara ya kwanza ya pamoja kati ya Jumuiya ya Afrika na Misri."

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Klabu ya Al-Tersana, Mohamed Tariq Saeed, alielezea furaha yake kwa ukarabati na ujenzi wa uwanja wa mpira wa kikapu katika Klabu ya Al-Tersana, Akisisitiza kuwa uwanja huo utavutia vijana mbalimbali kufanya mazoezi ya mpira wa kikapu, na kueneza uelewa kwa vijana kuhusu mpira wa kikapu na athari zake kwa afya na maendeleo ya jamii.

Itifaki hiyo ilitiwa saini na Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Ashraf Sobhy, na Mark Tatum,  Naibu Kamishna wa NBA Afrik

Comments