Dokta Ashraf Sobhy ni Mzungumzaji kwenye kikao kinachoitwa "Vijana katika 2030" wakati wa mkutano wa vijana katika Baraza la kiuchumi na la kijamii kwa Umoja wa Mataifa
- 2022-04-25 00:33:31
Sobhy: Rais El-Sisi anawasaidia Vijana na anawaangalia kwenye Vipaumbele muhimu zaidi
Waziri wa Vijana na Michezo: Misri yawekeza uwezo wa vijana na kuwatia hamasa kwa uvumbuzi na ubunifu
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Mkuu wa Ofisi wa Kiutekelezaji kwa Baraza la Mawaziri Waarabu wa Vijana na Michezo alishiriki katika kikao cha "Vijana katika 2030: kufikia malengo ya Maendeleo Endelevu ni pamoja na Vijana na kwa ajili yao"
wakati wa mkutano wa Vijana kwa Baraza la kiuchumi na kijamii kwa Umoja wa Mataifa.
Waziri huyo, wakati wa kikao hicho, aliwakaribisha wote walioshiriki kama wajumbe wa serikali na vijana wanaotenda katika kazi ya umma, ya kikanda na ya kimataifa katika mkutano huo.
Waziri huyo alisema :" sote tuliishi na bado tunaishi kipindi miongoni mwa vipindi vigumu zaidi vya historia mpya wakati wa Ulimwengu wote kukumbwa na athari za Janga la Corona ambalo lilisababisha vifo vingi vya watu na athari nzito za kiuchumi na kijamii, na liliwashinda vijana ambapo liliathiri kwa kiwango kikubwa nafasi zao za kutendana na matatizo ya jamii".
Aliongeza akisema :" serikali zote za Dunia zilijaribu na bado zinajaribu kuwapunguza wananchi wao mizigo sawa iwe ya kiuchumi, ya afya, ya kinafsi au mengineyo, kwa hiyo ni lazima siku zijazo kunufaika kwa uzoefu wa vijana na kuwatia mkono ili kukabiliana na changamoto hiyo ya kimataifa".
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba Misri, kwa Uongozi wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, imejaribu kuwaunga mkono Vijana, kuwaweka utangulizi wa vipaumbele na kuwekeza uwezo wao ambao ulichangia maendeleo ya jamii, akionesha kuwa Wizara wa Vijana na Michezo iliandaa mkakati wa kitaifa kwa Vijana na Wachipukizi 2022_2027 kwa ushirikiano pamoja na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa wakaazi na Chuo cha Kiarabu cha Sayansi, Teknolojia na cha Usafiri wa Baharini sambamba na mkakati wa Umoja wa Mataifa kwa Vijana 2030, mkakati wa kitaifa wa kimisri kwa Vijana na Wachipukizi unawakilisha msingi wa mahitaji na matakwa ya vijana kwa miaka mitano ijayo, isitoshe programu za maendeleo ya vijana na kuwaunga mkono , lililoifanya Misri kupanda na kushika nafasi ya 13 katika kielelezo cha Vijana Duniani.
Dkt. Ashraf Sobhy alionesha kuwa Wizara ya Vijana na Michezo inawaunga mkono Vijana kwa uvumbuzi, ubunifu na akili ya bandia kwa kupitia ubadilishaji wa majengo ya vijana ya kujifunzia ili kuwa vituo vya uvumbuzi vya vijana na kujifunza, vilevile kuongeza uandaaji wa vijana katika sekta ya elimu ya kifundi, warsha za kazi, maendeleo ya kibinafsi, usimamizi wa wakati na pia vikao vya mafunzo ili kuendeleza ustadi wa maisha, mbali na kuzingatia uwezeshaji kiuchumi kwa vijana na kuboresha aina ya kazi kupitia kueneza Utamaduni wa kazi ya kujitegemea, kuwawezesha vijana kwa Soko la Ajira na kuimarisha mafunzo katika miradi midogo, ya kati na Ujasiriamali.
Comments