Vijana na Michezo: washiriki 150 wako katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la tatu kwa Ufadhili wa Mheshimiwa Rais


Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy ilitangaza Ushiriki wa viongozi 150 kutoka kwa vijana wa nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi marafiki katika shughuli za kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa  Uongozi wa Kimataifa, Juni ijayo, kwa kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini na Vijana wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote", na hivyo pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.


Waziri wa Vijana na Michezo alithibitisha kuwa uongozi wa kisiasa nchini Misri ukiongozwa na Rais Abd El Fatah El-Sisi, una nia ya kusaidia na kuwarekebisha vijana kutoka mataifa mbalimbali Duniani kupitia Udhamini wa kuwezesha unaotolewa kutoka kwa Misri, pamoja na Udhamini maalum wa kiufundi. Unaotolewa na mashirika na Wizara za Misri,  inayochangia kufungua matarajio ya maendeleo na kuhamisha Uzoefu na tamaduni katika nyanja na Taalamu mbalimbali.


Toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa linalenga Viongozi 150 kutoka kwa vijana na wasichana wa Nchi Zisizofungamana kwa Upande Wowote na nchi marafiki kutoka kwa watoa maamuzi katika sekta ya umma, wahitimu wa Programu ya Wajitolea wa Umoja wa Afrika, viongozi watendaji katika sekta binafsi.


Wawakilishi wa matawi ya kitaifa ya Mtandao wa Vijana wa Harakati Zisizofungamana kwa Upande Wowote, wanaharakati wa taasisi za kiraia, wakuu wa mabaraza ya kitaifa ya vijana, wajumbe wa mabaraza ya mitaa, viongozi wa vyama vya vijana, wanachama wa Kitivo cha Chuo Kikuu, watafiti katika vituo vya utafiti wa kimkakati na mawazo, wanachama wa mashirika ya kitaaluma, wataalamu wa vyombo vya habari na waandishi wa habari, na wajasiriamali wa kijamii pia watashiriki katika Udhamini huo .

Comments