Waziri wa Michezo ashuhudia mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara na kampuni ya "TotalEnergies Egypt" ya kutunza ligi ya Vituo vya Vijana kwa Mpira wa Miguu
- 2022-05-04 21:07:55
Dkt. Ashraf Sobhy: alisema kuwa ligi ya Vituo vya Vijana inachangia ugunduzi wa talanta na maendeleo ya vituo vya vijana na wachezaji 108 waliohamia timu ya michezo kwa kupitia mashindano ya ligi hiyo.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ameshuhudia sherehe ya kusaini mkataba wa ushirikiano kati ya Wizara na kampuni "TotalEnergies Egypt" ili kukunza ligi ya vituo vya vijana na mashirika ya vijana, hivyo kwa mahudhurio ya Tomas Stroch Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya "TotalEnergies Egypt", na baadhi ya viongozi wa Wizara.
Katika hotuba yake, Dkt. Ashraf Sobhy, alisema:"mpango wa ligi ya Vituo vya Vijana kwa Mpira wa Miguu unajumuisha miradi ya maendeleo kwa vituo vya vijana wa Misri, moja ya malengo ya mradi huo ni kushughulikia maendeleo, uteuzi na vipaji katika mpira wa miguu, na kuchukua muda wa ziada wa vijana kupitia mazoezi, pamoja na msaada wa kiuchumi kupitia tuzo zinazotolewa na Wizara kwa vituo vya vijana vinavyoshiriki ligi hiyo kulingana na idadi ya pointi wanazozipata.
Waziri huyo alitoa Shukrani na Heshima kwa Kamati iandaayo Ligi, wale wanaohusika na utawala mkuu kwa vituo vya vijana na mashirika ya vijana, na utekelezaji wa ligi kwa ushirikiano na makurugenzi ya vijana na michezo katika mikoa mbalimbali, akizungumzia kipengele cha elimu ambacho Wizara inazingatia katika mashindano ya ligi na kuchukua hatua zinazohitajika, Na matumizi ya kanuni kuelekea kuondoka yoyote kutoka kwa maelezo.
Waziri huyo alieleza ushiriki wa wachezaji 17,100 wakiwakilisha timu 570 za vituo vya vijana katika Ligi ya mpira wa miguu ya Vituo vya Vijana inayotolewa hivi sasa, akibainisha kuwa kuna wachezaji 108 waliohamia timu ya michezo kupitia mashindano ya ligi hiyo, linalothibitisha kufanikiwa kwa malengo ya ligi hiyo. kwa ushirikiano na Total katika kutunza ligi hiyo kunatokana na nia ya kushirikiana na taasisi kubwa kutunza matukio na miradi mbalimbali ya vijana na michezo.
Dkt. Ashraf Sobhy, alieleza kuwa nguzo zote za maendeleo zipo kwa kuboresha, kuinua ufanisi na kuendeleza vituo vya vijana katika mikoa mbalimbali, na katika kipindi cha hivi karibuni vituo vya vijana 1051 vineanzishwa na kuendelezwa ndani ya mpango wa Rais " Maisha Bora" Pamoja na mradi wa kuendeleza viwanja vya mpira wa miguu na miradi ya uwekezaji katika vituo vya vijana kwa ushiriki wa sekta binafsi, ikionyesha mwelekeo wa wizara kugeuza vituo vya vijana kuwa vituo vya huduma kwa jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa "TotalEnergies Egypt" Tomas Stroch alizungumzia utunzaji wa Total wa michuano ya Mataifa ya Afrika 2019, na nia yake ya kutunza mashindano makubwa ya michezo, akionyesha nafasi ya Ligi ya Vituo vya Vijana katika kuibua vipaji na kutambua uhalali. ndoto ya vijana na watu wenye vipaji kuhitimu kama Mohamed Salah, kupongeza juhudi za Wizara ya Vijana na Michezo katika kuwakusanya vijana hawa kutoka mikoa mbalimbali.
Itifaki hiyo ilitiwa saini kutoka Wizara ya Vijana na Michezo na Meja Jenerali Ismail El Far, Mkurugenzi Mtendaji wa Wizara hiyo, na kwa upande wa Total, Mkurugenzi Mkuu wa "TotalEnergies Egypt" Tomas Stroch.
Comments