Misri yaandaa michuano ya 8 ya kupiga risasi ya Afrika juu ya sahani wazi za kuruka
- 2022-05-10 12:48:39
Misri inaandaa shughuli za michuano ya 8 ya kupiga risasi Afrika juu ya sahani vya wazi za kuruka, nayo ni michuano ya kufikia Kombe la Dunia la Shirikisho la kupiga risasi la Kimataifa, Kwa ushiriki wa wapiga risasi 250 wa kiume na wa kike na wachipukizi kutoka nchi 9 kutoka nchi mbalimbali za Dunia, michuano hiyo itaendelea kwa siku 4 kuanzia tarehe 12 hadi 15 Mei 2022.
Mashindano hayo yanakuja ndani ya michuano ya kufikia Fainali za Dunia za kupiga risasi, ikizingatiwa kuwa Misri imeandaa michuano 7 ya Afrika mnamo miaka iliyopita, mbali na kuandaa michuano miwili ya Dunia, ya mwisho ikiwa ni mwaka jana 2021, iliyoushangaza ulimwengu na kusifiwa na wapiga wote wanaoshiriki.
Michuano ya Afrika itafanyika katika viwanja vya kimataifa Klabu ya Risasi mnamo 6 Oktoba, iliyoidhinishwa na Kamati ya Kiufundi ya Shirikisho la kupiga risasi la Kimataifa tangu 2010, viwanja hivyo huandaa mashindano yote ya kategoria mbalimbali zinazoshiriki michuano hiyo, ambazo ni (waanzilishi wa zamani, waanzilishi, wanaume, wanawake, kiume wa wachipukizi na kiume na wa kike).Timu ya kwanza ya wapiga risasi wa Ulaya, timu ya kitaifa ya Italia na timu ya Kiingereza itashindana katika michuano hiyo, pamoja na ushiriki wa mabingwa wa nchi za Kiarabu na mabingwa wa Afrika.
Timu mashuhuri iliyoshinda nafasi za kimataifa wakati wa michuano iliyopita itashiriki katika michuano hiyo kutoka Misri na ambayo ni pamoja na uteuzi wa washambuliaji mahiri wa kimataifa kutoka klabu mbali mbali za Jamhuri, maarufu zaidi kati yao ni klabu ya Risasi huko Dokki, klabu ya Risasi huko Aleskandaria, klabu ya Shams, klabu ya Maadi, na klabu ya kuvua ya Wadi El-Natrun.
Kuhusiana na hilo, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alithibitisha kwamba Misri inaleta mabadiliko katika kuandaa hafla na michuano mbalimbali ya kimataifa kutokana na vipengele vyake vya michezo na Miundombinu iliyoanzishwa kwa mujibu wa viwango vya kimataifa.Alieleza kuwa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, alisisitiza upanuzi wa kujenga na kuendeleza vifaa vya michezo, ambavyo vimekuwa thamani ya ziada katika kusaidia uchumi wa kitaifa.
Sobhy alitathmini nafasi ya Shirikisho la kupiga risasi la Misri linaloongozwa na Meja Jenerali Hazem Hosni katika kuendeleza mchezo wa kupiga risasi na kupanua mazoezi huku akieleza kuwa Wizara itatoa msaada stahiki kwa ajili ya kufanikisha michuano hiyo ya Afrika.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Hazem Hosni, Rais wa Shirikisho la kupiga risasi la Afrika na Misri, Shukrani kwa Dkt. Ashraf Sobhy, kwa Ushirikiano endelevu wa Shirikisho hilo kwa mafanikio ya michuano hiyo, akibainisha kuwa michuano hiyo ina hadhi maalum kwa Misri kwa sababu ya umuhimu wake wa kimichezo wa kimataifa na Afrika katika uwanja wa upigaji risasi, alisisitiza kuwa kuandaa mchuano huo ni heshima kubwa kwa michezo ya Misri na ujumbe mzito chanya kwa taasisi zote za michezo Duniani, baada ya Misri kupata heshima ya Dunia nzima kwa kuandaa michuano ya Dunia mwaka uliopita.
Comments