Waziri wa Michezo awapongeza Mabingwa wa Mradi wa bingwa wa Olimpiki na Vipaji katika Kuinua Uzito katika Ushiriki wa Kwanza wa Kimataifa Nchini Ugiriki
- 2022-05-10 12:50:33
DKT.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Mchezo, aliwapongeza mabingwa wote wa mradi wa kitaifa wa bingwa wa olimpiki, vipaji na wafuasi wake, haswa mchezaji Mohamed Abdel Moneim Sayed aliyepata nafasi ya nne katika mashindano ya Dunia ya wachipukizi, chini ya umri 20 katika kuinua Uzito, yanayokaribishwa kwa Ugiriki mnamo kipindi cha 1 hadi 11 Mei hii.
Hii ni ushiriki wa kwanza wa kimataifa wa wachezaji wa kuinua Uzito wa mradi wa kitaifa wa vipaji na bingwa wa olimpiki kwa wachezaji watano, ni Mahmuod Hosny ( Mkoa wa Kairo), Mahmuod Gamal ( Mkoa wa Fayoum), Mohamed Abdel Moneim Fadel ( Mkoa wa Beni Suef), Helmy Abdel Bari ( Mkoa wa Ismailia ), Nora Essam Helmy( Mkoa wa Isamilia).
Wizara wa vijana na mchezo inatekeleza mradi wa kitaifa wa binga wa olimpiki na vipaji ndani ya mikoa yote ya Jamhuri, ili kugandua na kutunza wenye vipaji katika michezo ya " Ndondi, Mieleka, Judo, Taekwondo,Riadha, Tenisi ya Meza, Mpira wa Vikapu, Mpira wa Mikono na Kuinua Uzito" na kuongezeka kwa mradi wa kitaifa wa wenye vipaji wa Squash.
DKT.Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba Rais Abd El Fatah El_ Sisi anatoa msaada wote kwa mchezo, hii ni motisha kwa kila mtu ili kufikia maendeleo na mafanikio ya michezo ya kimisri, akielezea kwamba mradi huo wa kitaifa wa vipaji na bingwa wa olimpiki ni mhimili wa timu kupitia kikundi cha viwango ili kuchagua wenye vipaji katika mikoa yote kulingana na mpango maalumu wa kazi, na kuwajumuishwa katika mradi huo, uandalizi wa kuwatayarisha na kuwafikisha mashindano mbalimbali katika hatua za mradi zinawakiliswa katika hatua hizo mbili "wachipukizi, wa kesho " kufikia hadi hatua ya bingwa na kuiwasilisha kwa klabu za michezo na timu za kitaifa.
Waziri huyo aliashiria kwamba ujumbe wetu katika mradi huo ni ujumbe wa elimu, kitaifa, kisanii na michezo, tunatenga bajeti kubwa pamoja na kushughulikia kuendeleza Rasiliamali za mradi, akionyesha jukumu la kamati ya kisayansi na ya kifundi ya mradi huo, pia ufuatiliaji na Tathmini ya mara kwa mara ya matokeo yaliyopatikana kwa malengo yanayotarajiwa.
Comments