Waziri wa Michezo atafuta ushirikiano na Rais wa Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo


Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhy, alikutana na Mkuu wa Ofisi ya Utendaji ya Baraza la Mawaziri wa Vijana wa Kiarabu na Michezo, Jumapili asubuhi, ofisini mwake katika Ofisi ya Wizara,  Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo, Mohamed Hamad Al-Hanzab, kwa kutafuta ushirikiano baina ya nchi hizo mnamo kipindi kijacho.


Waziri huyo alisikiliza muhtasari kuhusu jukumu la Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo, kilichoanzishwa nchini Qatar mwaka 2011, na kinalenga kusaidia na kuimarisha Usalama na Amani katika uwanja wa michezo, na kuchangia kushughulikia kwa bidii shida zinazofaa,na kutoa huduma za mafunzo na ushauri kwa usalama wa michezo katika shughuli zake zote za michezo.


Waziri huyo aliwasilisha uzoefu wa kimisri katika kupata viwanja vya michezo wakati wa michuano ya Afrika iliyoandaliwa na Misri mwaka 2019, kwa msaada wa kundi la vijana, na hatua mbalimbali za mafunzo walizozipitia, pamoja na kufanikisha mashindano yaliyoandaliwa na Misri, na vifaa vya vijana na michezo katika ngazi ya serikali.


Dkt. Ashraf Sobhy alitoa wito wa maandalizi ya kufanya mkutano mwingine mnamo kipindi kijacho, kwa mahudhurio ya viongozi wa CAF, kujadili faili la Usalama wa michezo na taratibu za utekelezaji wake kwa mujibu wa mfumo maalum katika ngazi ya bara la kiafrika, na kuchangia kuanzishwa kwa kongamano la usalama na usalama wa michezo katika viwanja vya Afrika, Akibainisha kuwa masharti ya ushirikiano na Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo yamefafanuliwa, na vifungu hivyo viliwekwa katika itifaki ya ushirikiano katika maandalizi ya kusainiwa.


Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo alisisitiza umuhimu wa nafasi ya Misri katika eneo, na ushawishi wake mkubwa wakati iko katika ubora wake, na kwamba Misri ina uwezo wa kupata mafanikio makubwa katika ngazi ya uchumi wa michezo, Akielezea nia yake ya kushirikiana na Wizara ya Vijana na Michezo, na kujadili uwezekano wa kuanzisha tawi la Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo huko Kairo.


Pia, ilikubaliwa kuwa Kituo cha Kimataifa cha Usalama wa Michezo kitawasilisha karatasi kazi kuhusu Usalama na Amani wa michezo, itakayojadiliwa wakati wa mkutano wa Baraza la Mawaziri wa Vijana wa Kiarabu na Michezo uliopangwa kufanyika mwishoni mwa Mei hii. 

Comments