Sobhy akutana na Vijana watafiti walioteuliwa kuwakilisha Misri katika Jukwaa la London la Wanasayansi Vijana LIYSF
- 2022-05-13 20:48:32
Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikutana na Vijana Watafiti waliochaguliwa kuiwakilisha Jamhuri ya kiarabu ya Misri huko Kongamano la London la Wanasayansi LIYSF, linalokaribishwa kwa Chuo Kikuu cha Amperial College London, Marekani,mnamo kipindi cha Julai 27 hadi Agosti 17, 2022.
Waziri huyo alithibitisha kuwa Misri inafanya jitihada kubwa za kuwaendeleza vijana katika nyanja mbalimbali, kuvumbua na kuibua vipaji, kuviboresha na kuviendeleza ili kutumikia nchi na jamii, akiashiria umakini wa Wizara ya Vijana na Michezo kuwaenzi na kuwahamasisha vijana mashuhuri katika nyanja mbalimbali.
Dkt Ashraf Sobhy alielekeza lazima ya kutoa mahitaji yote ya vijana hao kabla na wakati wa ushiriki wao katika kongamano hilo, akiwatakia mafanikio na kupata mafanikio ya kisayansi kwa ajili yao na nchi yao pia.
LIYSF ni kongamano la sayansi linalofanyika katika Chuo cha Imperial London nchini Marekani, ambapo zaidi ya wanasayansi vijana 500 kutoka nchi zaidi ya 50 zinazoshiriki hushiriki, na inajumuisha mihadhara na mikutano kadhaa na wanasayansi wakuu kutoka kote ulimwenguni, kutembelea viwanda na vituo vya utafiti na taasisi za kisayansi, ikijumuisha ushindani mkubwa kati ya wanafunzi kuwasilisha mawazo na ubunifu unaofanya kazi kuendeleza ulimwengu.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Dkt.Abdullah Al-Batish, Waziri Msaidizi mkuu wa Sera na Maendeleo ya Vijana, Ahmed Afifi, Mkuu wa Idara Kuu ya Bunge na Elimu ya Uraia, na Mustafa Magdy, Waziri Msaidizi wa Sera na Maendeleo ya Vijana.
Inaashiriwa kuwa vijana hao ni "Mohamed Alaa El-Din, Abdel-Rahman Metwally, Hadeer Abu Al-Saud, Esraa Al-Hassanin", wanaowakilisha Vyuo Vikuu vya "Misri kwa Sayansi na Teknolojia, Helwan, na Mfereji wa Suez".
Comments