Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unazindua sherehe ya ufunguzi wa toleo lake la tatu

Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unazindua sherehe ya ufunguzi wa toleo lake la tatu, ambayo umeandaliwa ikiwa na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi, kwa kushirikiana kwa viongozi  vijana 150 kutoka nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, ambayo imepangwa kuendelea hadi Juni 17, 2022 katika Mahali pa Shirika la Uhandisi huko Kairo, pamoja na kauli mbiu " Vijana wasiofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini_ Kusini.

Ufunguzi huo umezinduliwa kwa mahudhurio ya Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy, Balozi  Amr Moussa ambaye ni mjumbe wa kamati ya majaji ya Umoja wa Afrika , Waziri wa zamani sana wa Mambo ya Nje ,Katibu mkuu wa zamani sana wa Jumuiya ya Nchi za kiarabu,  Dkt.Mostafa E l-Feki Mkuu wa Maktaba ya Aleksandra, Konsela na katibu mkuu wa baraza la bunge " Ahmed Manaa" , Balozi na msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje " Ehab Badwy" , Mwandishi wa habari " Karam Gabr ambaye ni mkuu wa baraza kuu la kuandaa vyombo vya habari , Meja Jenerali " Isamail Al_Far ambaye ni mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Vijana na michezo, Mbunge wa baraza la wawakilishi " Mahmoud Hussien" ,  mkuu wa kamati ya Wizara ya Vijana na michezo , na viongozi wengi wa mabaraza ya wawakilishi, Seneti, Mabalozi, Watu mashuhuri katika jamii , wanasiasa, wanahabari, wakuu wa vyuo vikuu, viongozi wa nchi ya Misri, uratibu wa vijana ya vyama na wanasiasa, viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo ,na wawakilishi wa vipande vinavyoshiriki.

Mheshimiwa mwanahabari " Mohamed Turk" ameshughulikia sherehe ya vyombo vya habari na pia mwanahabari Dkt, Yasser Abdelaziz alidhibiti kikao cha mazungumzo cha Dkt, Amr Moussa kwa kauli mbiu " Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, na mwingiliano wa kimataifa"

Comments