Kikao cha majadiliano kuhusu Waanzilishi wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote katika ufunguzi wa shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
- 2022-06-23 12:06:17
Wizara ya Vijana na Michezo ilizindua shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa- kundi la tatu, linaloandaliwa pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kupitia kikao cha mazungumzo kwa ushirikiano wa viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi marafiki,unaoandaliwa mnamo kipindi cha kuanzia tarehe 31 Mei hadi 17 Juni , 2022 kwenye Jumba la Mamlaka ya Uhandisi mjini Kairo. na hayo kwa kauli mbiu "Vijana wa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini".
Kikao hicho cha mazungumzo katika ufunguzi wa shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa katika toleo lake la tatu kilihudhuriwa na Balozi Dominic Goh, Balozi wa Singapore nchini Misri, Balozi Ajit Gupti, Balozi wa India nchini Misri, na Dkt. Ahmed Youssef Ahmed, Mkuu wa zamani sana wa Taasisi ya Tafiti na Mafunzo ya Kiarabu, kilichokuja kikiwa na kichwa cha habari "Waanzilishi wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote - Kuangalia maisha yenyewe", na kilisimamishwa na Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa .
Balozi wa india wakati wa kikao cha kwanza cha mazungumzo ya shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akizungumzia jukumu la kiongozi Nehru katika harakati ya kutofungamana kwa upande wowote , akionesha uhusiano mkubwa kati ya kiongozi wa India Nehru na Rais Gamal Abdel Nasser, akieleza kwamba India imekuwa na mchango mkubwa katika kuanzisha harakati hiyo . vilevile , India iliunga mkono kwa nchi nyingi na imekuwa yenye ushirikiano chanya , ambapo India haikupata nguvu kutoka viongozi wake tu , bali wapo viongozi wengi katika bara la Afrika walioathirika katika utu wao kama Nelson Mandela na Gamal Abdel Nasser, na alisisitiza kuwa licha ya shinikizo walilokumbana nalo nchini India, ila Walilinda uhuru wao wa kiuchumi na wa kifikra kupitia kufuata sera ya uhuru wa kimkakati iliyochorwa na watangulizi wao, na walianzisha ushirikiano na nchi nyingi za kimataifa , nchi za ulimwengu zimekuwa zikitamani kiwa na mahusiano kadha ya kiuchumi , kisiasa na kiutamaduni pamoja na nchi mbalimbali ambazo zimekuwa zimetamani mnamo Mwaka 2030 kwamba India iwe miongoni mwa nchi zinazoshindana Katika ulimwengu wa anga za juu ambapo hawakuzingatia tu uchumi lakini pia wana mashirikiano katika sekta ya wa elimu , pamoja na kuwepo kwa maprofesa wengi wa vyuo vikuu kutoka India ambao wana mashirikiano mazuri katika vyuo vikuu vyote ulimwenguni .
Balozi wa Singapore wakati wa hotuba yake katika kikao cha ufunguzi wa siku ya tatu ya udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alionesha uhusika wa kiongozi l" Le kongh Yo " katika harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, akibainisha kuwa ulimwengu umebadilika sana haswa na harakati ya mapinduzi, ambapo kulikuwa na ubaguzi mkubwa wa rangi na kikabila licha ya kile kilichosababishwa na ukoloni kutoka uhalifu ndani ya nchi .Balozi wa India aliongeza kusema kuwa Lee Kuang Yew alikuwa na akitilia mkazo sana kwa kujua jinsi ulimwengu unavyoendelea na kufaidika na uzoefu huo katika nchi yake na aliamua kutegemea viwanda na sicho kilimo tu, akieleza kuwa Singapore ilikuwa na baadhi ya harakati za kigaidi zilizojitokeza, jambo ambalo lililetea changamoto ili kuendeleza nchi hizi, na kwamba Lee Kuang Yew, alizungumza na Gamal Abdel Nasser na viongozi wengine na alikata uamuzi kwamba Singapore lazima ijiunge na harakati ya kutofungamana kwa upande wowote ili kulinda mamlaka na uhuru wao, akisisitiza kuwa tunapozungumzia maendeleo na kuunda fursa kwa wananchi ili kuendeleza , Hilo lilichukua muda mrefu ili waweze kupata uzoefu na kupiga hatua kwa haraka wakati huohuo. hilo ndilo lililowafanya sasa hivi waweze kukaribisha mataifa ya kigeni ili kuwekeza nchini mwao, haswa wakati wa umakini wao wa kuunda Amani ya ndani ili wajisikie Usalama na Amani inayohitajika kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kuunga mkono wa uwekezaji katika nchi zao.
Dkt. Ahmed Youssef Ahmed, Mkuu wa zamani sana wa Taasisi ya Tafiti na Mafunzo ya kiarabu ,mwanzoni mwa hotuba yake katika ufunguzi wa kikao cha shughuli za siku ya tatu ya Udhamini wa Uongozi wa Kimataifa wa Nasser, alitoa Shukrani kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa mwaliko wa kushiriki katika Udhamini huo muhimu unaopewa jina la kiongozi wa Misri Gamal Abdel Nasser, akizingatia kuwa Udhamini huu ni kama mwanzo wa Harakati ya vijana ya kimataifa ambayo inafanya kazi kwa ajili ya maendeleo, "Youssef" alizungumzia nafasi ya Gamal Abdel Nasser katika harakati ya kutofungamana kwa upande wowote akieleza kwamba harakati isiyofungamana kwa upande wowote ilianza harakati ya kimataifa ambapo Gamal Abdel Nasser alichangia katika harakati ya kutofungamana kwa upande wowote tangu mwanzoni mwa harakati hiyo .
Hatuwezi kuelewa kuibuka kwa wazo la Harakati hiyo kwa kiongozi Gamal Abdel Nasser bila kuiweka katika muktadha wa wakati na mahali alipokulia ambapo alikua kwenye mahali ambapo palimsaidia kuelewa thamani ya Uhuru , na katika muktadha wa sifa zake zisizo za kifani na zinazohusiana na jinsi ya kutetea Uhuru , kushikilia hadhi ya kitaifa pamoja na Umuhimu wa kujua asili ya wazo la haraka kutofungamana upande wowote na tuwe na mitazamo chanya inayoendana na masilahi ya kitaifa kwa raia , kiini cha wazo la kutofungamana kwa upande wowote kwake , Gamal Abdel Nasser na Ujumla wa wazo hilo kwa mtazamo wake , ambapo amani na ukombozi ulikuwa dhana za msingi kwake na kila mara alikuwa akizingatia hitaji la kukamilisha mchakato wa kihistoria wa kuondoa ukoloni na tawala za kikoloni katika nchi hata hivyo, alitilia mkazo pia masuala ya maendeleo katika nchi, na aligusa asili ya wazo la kutofungamana kwa upande wowote ambapo Nasser alikuwa akisisitiza haraka ya kutoelekea na upande wowote sio upande wa tatu, bali ni kwa ajili ya kupunguza mvutano kati ya pande hizo mbili na sio kwa ajili kushawishi migogoro kati yao ili kutafuta faida kubwa zaidi Lakini inataka ukaribu kati yao .
Bw.Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alieleza kuwa Udhamini huo ulichukua jina la Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser, ikizingatiwa kuwa yeye ni mmojawapo wa viongozi muhimu kwa raia wa nchi zinazoendelea (Afrika - Asia - Amerika ya Kusini) na mmojawapo wa mifano muhimu ya kipekee ya uongozi ambapo anaitwa "" Baba wa Afrika." vilevile ,Rais Gamal Abdel Nasser ni mfano safi na mfano wa kisiasa na kihistoria wa dhana ya uongozi kutokana na nafasi yake, kama kiongozi aliyetilia mkazo kwa kuunga mkono harakati za ukombozi wa kimataifa hadi kupata uhuru wao, na pia alichangia kwa nguvu katika kuanzisha mashirika yaliyowaunganisha raia wa mabara (Asia - Afrika - Marekani ya kusini ) nayo ni shirika la Mshikamano wa Watu wa Asia, Afrika , Marekani ya kusini ) , Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu.
Ghazaly aliongeza kuwa, Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , katika toleo lake la tatu, unakuja kwa ushiriki wa viongozi vijana wanaowakilisha takriban nchi 73 ulimwenguni kote, pamoja na wajumbe wa Misri, wanaowakilisha makundi mengi ya kijamii yaliyolengwa na Udhamini mwaka huu, ikiwa ni pamoja na makundi ya kitaifa kwa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote , na wakuu wa mabaraza ya kitaifa ya Vijana , wanachama wa mabaraza ya ndani , watafiti katika vituo vya utafiti wa kimkakati na mawazo, pamoja na wanachama wa mashirika ya kitaaluma, pamoja watangazaji wa vyombo vya habari, waandishi wa habari na wajasiriamali wa kijamii.
Comments