Kikao cha mazungumzo kuhusu Kutaifisha Mfereji wa Suez ni Hadithi ya Watu Mwishoni mwa shughuli za siku ya nne ya Udhamini
- 2022-06-23 12:12:27
Wizara ya Vijana na Michezo iliandaa, Jumamosi jioni, Kikao cha mazungumzo yenye kichwa "Kutaifishwa kwa Mfereji wa Suez ni Hadithi ya Watu" kwa mahudhurio ya Naibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Taifa katika Seneti, Meja Jenerali Tariq Naseer,na mtaalamu na mwanahistoria, Dkt. Ali Al-Hefnawi, na Mhakiki wa Sanaa Bw.Mohamed El Rubi, profesa wa Jukwaa kwenye Chuo kikuu cha Sanaa za kienyeji na mhariri mkuu wa gazeti la Jukwaa letu, Kikao hicho kilisimamishwa na mwandishi wa habari na mkurugenzi wa kitengo cha maandishi katika chaneli ya DMC, Bw.Ahmed Al-Derini.
Na hiyo ilitokea katika hitimisho la shughuli za siku ya nne ya Udhamini wa Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, linaloandaliwa pamoja na Ufadhili wa Rais wa Jamhuri,Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi,kwa ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki,pia itayofanyika mnamo kipindi cha kuanzia Mei 31 hadi Juni 17, 2022 katika Jumba la Mamlaka ya Uhandisi mjini Kairo pamoja na kauli mbiu ya “Vijana wa kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini."
Kwa upande wake, mwanafikra na mwanahistoria, Dkt. Ali Al-Hefnawi, katika hotuba yake wakati wa kikao cha mwisho cha mazungumzo ya shughuli za siku ya nne ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alizungumzia Historia fupi ya asili ya Mfereji wa Suez na umuhimu wake katika historia ya Misri,ikipitia historia ya kuibuka kwa Mfereji wa Suez kutokana na kuchimba hadi Marehemu Rais Gamal Abdel Nasser aliutaifisha, na akieleza kuwa Mfereji wa Suez ni kitovu muhimu na umekuwa chanzo cha vita vingi. Na kwamba wazo la kuchimba Mfereji wa Suez halikuwa wazo geni, bali lilikuwa ni wazo la kudumu na endelevu,Na ilipochimbuliwa, ikawa njia ya mabishano kati ya mamlaka kuu za wakati huo. Na Al-Hefnawi ameongeza kuwa hitaji la Misri kurejesha mfereji wa Suez lilikuwepo tangu wakati wa uvamizi wa Uingereza, na harakati zote za kitaifa za Misri zilipodai kurejeshwa kwa Mfereji wa Suez, na alikuwa wa kwanza kutumia neno kutaifisha Mfereji wa Suez, Talaat Harb katika kitabu kilichochapishwa mnamo 1910, na hitaji la kurejesha Mfereji wa Suez lilikuwa hitaji muhimu maarufu na la kitaifa tangu nyakati za zamani hadi urejesho wake ulipotaifishwa. Wakati wa enzi za Marehemu Rais Gamal Abdel Nasser, ikiwa ni utekelezaji wa dhamira ya raia wa Misri kuhusiana na suala hilo, ndipo ikaja taswira ya kuhifadhi mfereji wa Suez baada ya kutaifishwa tangu wakati wake hadi sasa, na kusababisha kuchimbwa kwa mfereji mpya wa Suez wakati wa enzi ya Rais wa Jamhuri,Rais El-Sisi.
Na Mkosoaji wa sanaa, Profesa wa ukumbi wa michezo katika Taasisi ya Juu ya sanaa ya kienyeji na mhariri mkuu gazeti la Jukwaa letu,Mohammed Al-Ruby, Mwanzoni mwa hotuba yake wakati wa kikao cha mwisho cha mazungumzo ya shughuli za siku ya nne ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu,alitoa Shukrani kwa Wizara ya Vijana na Michezo kwa mwaliko huo kwa kukutana na viongozi vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akisisitiza kwamba kuna umuhimu kwa sababu sanaa ya kila aina inahusika na matukio muhimu katika historia ya mataifa, haswa matukio muhimu na mfereji wa Suez, iwe kwa kuchimba au kutaifishwa. Baadaye, ni matukio mawili tofauti katika historia ya Misri, eneo zima, na hata ulimwengu mzima. Na Al-Rubi aliashiria Filamu ya Nasser 56, iliyotolewa kwa athari ya ulimwengu wa Magharibi kwa uamuzi wa kutaifisha na vita vya 56, Akieleza kuwa kushindwa au ushindi hupimwa kwa kiwango ambacho lengo la kijeshi lilifikiwa au kushindwa, ndilo lililokuwa lengo katika vita vya mwaka 1956, ilivyokuwa ni kwa rais wa Misri arudi nyuma kutaifisha.Na vita hii iishe wakati hakuna kurudi nyuma ni ushindi mkubwa kwa Misri, licha ya hasara iliyotokea kwa upande wa Misri.Al-Ruby aliwaalika washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwa ajili ya kutazama sinema ya "Port Said," iliyorekodiwa kuhusu vita vya 1956. Wakati wa kuzuka kwa vita hivyo, alitaja hadithi ya utayarishaji na upigaji picha wa sinema hii iliyosimuliwa na msanii Farid Shawqi katika shajara yake, ilipotokana na mwaliko, hamu na msaada wa Rais Gamal Abdel Nasser, aliyeona wakati wa kuzuka kwa vita umuhimu wa kutengeneza filamu inayoonyesha wakati wa vita huko Port Said kuhusu mateso ya watu huko Port Said wakati wa vita, na inadhihirisha mazoea ya adui dhidi yao katika vita.
Na Naibu wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa Kitaifa katika Seneti, Meja Jenerali Tariq Nassir, wakati wa hotuba yake kwenye kikao cha mwisho cha mazungumzo ya shughuli za siku ya nne ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo la tatu kwa aliwakaribisha washiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akitoa Shukrani kwa uongozi wa kisiasa wa Misri kwa kuandaa Udhamini huo muhimu, unaoshikilia ufadhili wa ukarimu wa Rais Abd El Fattah El-Sisi, akiashiria kuwa taifa la Misri kama limekuwa likilengwa mara kwa mara kwa sababu ya faida nyingi ndani yake na eneo bora zaidi, wakati Misri inapatanisha nchi za dunia na imekuwa ikilenga mfereji wa Suez kwa mamia ya miaka kwa sababu ni muhimu sana kwa Misri, Haswa katika muktadha wa kuhifadhi usalama wake wa kitaifa na kama rasilimali muhimu na ateri kwa serikali ya Misri na mapato makubwa zaidi ya kitaifa kwa Misri na Wamisri, Na akisifu Hadithi kubwa ya kienyeji ambayo haijawahi kutokea, iliyofanyika katika uchimbaji wa Mfereji mpya wa Suez uliofanyika wakati wa zama za Rais wa Jamhuri, Rais Abd El Fatah El-Sisi, na ushiriki wa Wamisri ndani yake na msimamo wao na nchi zao katika wakati wa shida.
Washiriki katika toleo la tatu la " Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" walitoa maswali kadhaa, na maelezo, na uingiliaji kati wakati wa kikao cha mazungumzo ya kufunga kutoka kwa shughuli za siku ya nne ya Udhamini, na hiyo ilikuja kuhusu kutaifishwa kwa Mfereji wa Suez, Kisha washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipiga picha za ukumbusho huku kukiwa na mwingiliano na makaribisho ya motomoto na furaha kutoka kwa wote , na katika kikao hiki mashuhuri na habari muhimu waliyopata kupitia kipindi hicho muhimu cha mazungumzo kuhusu Hadithi ya kienyeji kwa kutaifishwa kwa Mfereji wa Suez.
Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alibainisha kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu wa kale wa Misri katika kuunganisha na kujenga taasisi za kitaifa pamoja na kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka nchi za kutofungamana kwa upande wowote wenye maoni yanayoendana na ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la kihistoria la Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na jukumu lake mnamo siku zijazo, Mbali na kuanzisha jukumu la Mtandao wa Vijana wa Nchi Wanachama wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote(NYN), Na kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa katika ngazi ya nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki.
Ghazali aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa inatoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili kama lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 linavyoonyesha, Pia inawawezesha vijana na kutoa fursa kwa waigizaji kutoka nchi mbalimbali Duniani kuchangamana, na kuanzisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na si tu katika ngazi ya kibara, bali katika ngazi ya kimataifa kama lengo la kumi na saba la malengo ya maendeleo endelevu linavyoonyesha.
Ni vyema kutajwa kuwa, Leo, warsha iliandaliwa kama sehemu ya shughuli za siku ya nne ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu ikiwa na kichwa "Elimu na Uhamaji wa kijamii », ambapo uzoefu katika mashirika ya kiraia ulibadilishana kati ya washiriki kutoka nchi mbalimbali katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu.
Comments