"Mkuu wa Chuo cha Polisi" awapokea wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Leo, Jumatatu,Chuo cha Polisi, iliwapokea wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, miongoni mwa shughuli za siku ya sita ya Udhamini, unaoandaliwa pamoja na Ufadhili  wa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El Sisi, Rais wa Jamhuri, mnamo kipindi kuanzia Mei 31 hadi Juni 17, 2022 kwenye Jengo la Mamlaka ya Uhandisi jijini Kairo, kwa kauli mbiu "Vijana wa nchi za kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini".

Washiriki wa Udhamini huo katika toleo la tatu, walipokelewa na Jenerali Hani Abu Al-Makarem, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Chuo cha Polisi na idadi ya viongozi wa Chuo hicho pamoja na mahudhurio ya Bw.Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Jenerali Hani Abu Al-Makarem, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Chuo cha Polisi, aliwakaribisha wanachama wa wajumbe wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akiwapa salamu za Jenerali Mahmoud Tawfiq, Waziri wa Mambo ya Ndani, anayetoa uangalifu mkubwa kwa shughuli za ziara hii kutokana na ufahamu timamu wa jukumu la Misri la uongozi la na historia yake na kile kinachowakilishwa kwa ziara hiyo, inayoandaliwa ndani ya mkakati muhimu wa Wizara ya Mambo ya Ndani unaolenga kuimarisha ushirikiano na kujenga madaraja ya mawasiliano na taasisi na mashirika yote Duniani kote pia inazingatiwa mfano halisi wa ushirikiano uliopo kati ya Wizara mbili za Mambo ya Ndani na Vijana na Michezo katika uwanja wa kuwafundisha makada wa vijana kutoka nchi mbalimbali ulimwenguni, unaochangia katika kuimarisha mifumo ya ushirikiano kati ya Misri na nchi za mabara manne zinazoshiriki katika shughuli za Udhamini.

Shughuli za ziara ya wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kwenye Chuo cha Polisi, zilijumuisha kutazama filamu iliyosajiliwa ikionesha shughuli za Chuo pamoja na vyombo vyake mbalimbali ikifuatiwa na ziara ya ukaguzi ndani ya Chuo kupitia kwake washiriki katika Udhamini huo walitembelea shughuli na majengo ya Chuo na uwezekano wake ulioifanya mbele ya taasisi zinazohusika na mazoezi maalumu ya usalama kwenye viwango viwili vya kikanda na kimataifa pia ziara ya wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo kwenye Chuo cha Polisi, ilijumuisha kuzuru kituo cha utafiti cha polisi ambapo kutambua kozi ya mazoezi ya makada wageni wa askari wanaokuja kutoka nchi za kiafrika na nchi jirani za kigeni  na shughuli zake za utafiti wa polisi kwa mujibu wa kuwa chombo maalum cha kisayansi kwenye Wizara pamoja na kutembelea kituo cha Misri kwa mazoezi juu ya opresheni za kulinda Amani zinazofuata kitivo cha mazoezi na maendeleo na kinachofanya kazi  juu ya kuandaa Makada wa Usalama wa kitaifa na wa kigeni wanaofuata shirika la Umoja wa Mataifa kushiriki katika jumbe za kulinda Amani, pia kitivo cha masomo ya juu kwa kuwa taasisi ya elimu ya Usalama ya kipekee katika kiwango cha mashariki ya kati katika kuwapa wanaotaka kutoka kwa maafisa kujiunga na diploma zake vyeti vya kuthibitishwa kwa masomo ya juu ya usalama wa shahada ya kwanza (Uzamili, Uzamivu), na kitivo cha Polisi ambapo walitambua jitihada zilizofanywa katika kuandaa na kurekebisha mwanafunzi wa kitivo cha Polisi kwa mtindo bora wa kisasa na ya kisayansi.

Ziara ya washiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu kwenye Chuo cha Polisi, ilijumuisha kutambua jukumu la vyombo vyote vya Chuo hicho kwa kutumia data za sayansi kuhakikisha ujumbe wa usalama ambapo majengo muhimu zaidi za mazoezi na elimu yaliyopo ndani ya chuo kilikaguliwa (uwanja wa changamoto na mazoezi ya mwili _ mjumuisho wa nyanja za mazoezi ya kupigana _  kujilinda _ uwanja wa mafunzo ya kiufundi juu ya utaalamu wa kazi katika mfumo wa kuiga, kuangalia maonesho ya wanafunzi katika ujuzi wa kubomoa na kuunganisha silaha, kuangalia maonesho ya kipekee ya utawala mkuu wa mazoezi ya wanafunzi wa usalama na kulinda), na kupiga picha za kumbukumbu na kusambaza zawadi kwa wageni wanaoshiriki katika ziara hiyo.

Washiriki wa toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walionesha Shukrani zao za dhati kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri, iliyowakilishwa na Chuo cha Polisi kwa mapokezi motomoto katika ziara hiyo, ambayo iliwawezesha kutambua jukumu la Chuo katika kuandaa na kurekebisha tabia za walinda usalama, haswa jukumu lao katika mazoezi ya makada wa usalama, huku wakisifu jukumu la kihistoria na la kipekee la Polisi, ambalo haliishii tu kwa kuandaa na kurekebisha tabia za maafisa katika ngazi ya kitaifa, bali pia inaendelea hadi kwa makada wa usalama kutoka nchi za kiarabu na kiafrika.

Kwa upande wake, Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani, Mkuu wa Chuo cha Polisi na viongozi wa Wizara hiyo kwa ziara hii, inayokuja ndani ya jukumu la Wizara ya Vijana na Michezo ili kuwajulisha vijana wa Dunia nzima kwa juhudi zilizofanywa ndani ya Chuo cha Polisi kuandaa na kurekebisha tabia za walinzi wa usalama wa kisasa kupitia kufuata mifumo na mbinu za hivi karibuni zaidi za kimataifa ambazo wanazisoma nje ya nchi, alisisitiza kuwa Misri ina uzoefu wa muda mrefu katika uanzishaji na ujenzi wa taasisi za kitaifa, na "Ghazali" aliwaita washiriki kusimama dakika moja ya maombolezi kwa ajili ya roho za mashahidi wa nchi, na kisha alitamka “Misri yaishi .. Misri yaishi”.

"Ghazali" aliashiria kuwa mnamo siku zijazo, safari na ziara nyingi zitaandaliwa miongoni mwa shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu Kuelekea maeneo mengi kwa kuwatambulisha wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo kwa mafanikio ya kisasa ya Misri katika nyanja mbalimbali pamoja na kuwaruhusu kusikiliza na kuona ustaarabu wa Misri na maeneo yake ya kale ya ajabu ya kuvutia mioyo na macho ya watu kutoka nchi mbalimbali za Dunia.

Inatajwa kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, unalenga kuunda kizazi cha viongozi wa vijana kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote, wenye maoni yanayolingana na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kufahamisha kwa jukumu la harakati ya kutofungamana kwa upande wowote kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la Harakati ya vijana wa nchi Wanachama katika Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote "NYN", na kuunganisha viongozi  vijana wenye ushawishi mkubwa zaidi katika Ngazi ya Nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki.

Comments