Viongozi wa Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi wanajadiliana pamoja na washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika siku yake ya nane
- 2022-06-28 12:51:03
Katika ufunguzi wa kwanza wa shughuli za siku ya nane ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Wizara ya Vijana na Michezo iliandaa kikao cha mazungumzo kikiwa na kichwa: "Jukumu la Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi", kimeshirikishwa na; Mkuu wa Idara Kuu ya Mipango ya Mikakati na Miradi katika Kituo cha Maelezo na Kukuza Maamuzi, Meja Jenerali Hamdi Helmy, na Mkuu wa Sekta ya Kudhibiti Migogoro na Misiba na kupunguza hatari katika kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi Meja Jenerali Mohamed Abdel Maqsoud, na Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Mipango Mikakati katika Kituo hicho hicho, Dkt. Reham Sadek, na Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Jamii katika Kituo hicho hicho Mhandisi. Walid Jado,na Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa,
Na Mkurugenzi wa Idara Kuu ya Mipango Mikakati katika Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi, Dkt. Reham Sadiq, alitoa mada ya kina kuhusu kuanzishwa kwa Kituo hicho mnamo 1985 kituo hicho kimeshuhudia mabadiliko mengi ili kuendana na mabadiliko ya jamii ya Misri iliyopitia, Sadiq aliongeza kuwa shughuli muhimu za Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi ni pamoja na uwazi na uwepo katika ngazi za ndani na kimataifa, na kusaidia watunga sera,na maendeleo ya mifumo na zana za mawasiliano ya kijamii, na kusaidia juhudi za mabadiliko ya kidijitali,na Kuunga mkono utayari wa serikali katika kupambana na misiba na migogoro, na maendeleo ya ndani kwa taasisi, pia katika hotuba yake alifafanua tuzo maarufu zaidi zilizopokelewa na kituo hicho.
Na upande wake, Meja Jenerali Hamdi Helmy, Mkuu wa Idara Kuu ya Mipango Mikakati na Miradi katika Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi, wakati wa hotuba yake, alifafanua changamoto zinazokabili vituo vya mawazo, ikiwa ni pamoja na ufadhili mdogo, haja ya kuendeleza uhusiano na watoa uamuzi, na maendeleo ya haraka ya teknolojia, na matokeo ya utupaji wa taarifa kadhaa na data kubwa, pia katika hotuba yake alizungumzia maoni ya Kituo hicho ambayo ni kama chombo cha kwanza cha wasomi mashuhuri ndani na kimataifa,na chenye ushawishi mkubwa zaidi kwenye miduara ya kufanya uamuzi kwa ajili ya kufikia maoni ya baadaye ya Misri, "Helmy" aliongeza kwamba mwelekeo wa kimkakati wa kituo hicho ni taasisi ya fikra inayofanya kazi kuunga mkono uundaji wa sera za umma kupitia uchunguzi wa kina wa masuala ya pande nyingi na kuanzishwa kwa njia mbadala na mawazo bunifu kwa kukabiliana na changamoto na kuendeleza juhudi za maendeleo kwa kushirikisha pande husika, na malengo ya kimkakati,na kupanua ubora wa kitaasisi wa kituo hicho, na maendeleo ya jamii ya maarifa na pia kukuza uundaji wa sera za umma, na kuunga mkono utayari wa serikali kudhibiti hatari za migogoro na misiba.
Mkuu wa Sekta ya Kudhibiti Migogoro na Misiba na kupunguza hatari katika kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi,Meja Jenerali Mohamed Abdel Maqsoud, wakati wa kauli yake alizungumzia mkakati wa Kituo hicho katika udhibiti wa migogoro na misiba, akieleza kuwa Dunia nzima inapitia majanga na hatari nyingi, kwa hivyo ni muhimu kwetu kuwa utayari wa kukabiliana na hatari au migogoro yoyote, na "Abdul-Maqsoud" aliongeza kuwa utunzaji mzuri wa migogoro na misiba unahakikisha uhifadhi wa maisha ya serikali, na pia kwa kulinda usalama wa nchi na raia, na kufikia ustawi wa kiuchumi wa watu, katika hotuba yake, pia aligusia namna taifa la Misri linavyoendeshwa kwa migogoro na misiba kadhaa yaliyotokea, na kufanya kazi ndani ya muktadha wa upangaji kimkakati katika hatua za kabla ya migogoro ambapo mpango wa kitaifa unapangwa na kutengenezwa kwa jinsi ya kukabiliana na migogoro. Tunapata hapo, kwa mfano, kamati ya juu ya kukabiliana na athari za virusi vya Corona, iliyosimamia ipasavyo janga lililoathiri ulimwengu wote kikubwa, iliyofanya athari za mzozo kwetu kuwa na madhara kidogo kuliko athari zake kwa nchi nyingi za ulimwengu.
Kwa upande wake, Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Jamii katika Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi , Dkt. Mhandisi Walid Jado, katika hotuba yake alizungumzia jukumu la nguzo ya mawasiliano ya jamii katika Kituo hicho kama mfano wa mchakato wa kuunganisha kituo na wasikilizaji kupitia njia na zana za kisasa kuhakikisha hilo, mawasiliano kama hayo ya jamii na kufikia lengo linalotakikana ndani ya mfumo na malengo ya Kituo cha Taarifa na kukuza Maamuzi, na mbali na kazi ya kituo hicho katika uwanja wa kukuza mawasiliano kwa kukuza uhusiano na jamii ya watafiti na washirika, ambapo hatuwezi kufanya chochote bila mawasiliano na kutafuta njia mpya za mawasiliano,pamoja na kuendeleza jukumu la ufahamu na kushiriki katika matukio na washirika wa kimataifa,Kikao hicho pia kilichoshuhudia kikundi cha majadiliano kwa washiriki wa Udhamini na wahadhiri; Washiriki waliuliza maswali kadhaa na maelezo na uingiliaji wakati wa kikao katikati ya mwingiliano, na furaha kwa kila mtu, kikao hiki mashuhuri na maelezo waliyopata.
Na upande wake, Nw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, alieleza kuwa Udhamini wa Nasser unatoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili kama lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030 linavyoonyesha,pia unawawezesha vijana na kutoa fursa kwa waigizaji kutoka nchi mbalimbali Duniani kuchangamana, na kuanzisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali, na si tu katika ngazi ya kibara, bali katika ngazi ya kimataifa kama lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu linavyoonyesha, akiongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, unalenga kuhamisha uzoefu wa kale wa Misri katika kuunganisha na kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka nchi za kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na ufahamu wa jukumu la Jumuiya ya Harakati za kutofungamana kwa upande wowote la kihistoria na jukumu lake la siku zijazo.
Ni vyema kutajwa kuwa Warsha iliandaliwa kwa ajili ya washiriki katika shughuli za Udhamini kuhusu "Jukumu la Wanawake" katika mfumo wa warsha za programu ya "Raia wa Ulimwengu mzima" pamoja na usimamizi wa mkufunzi Ahmed Negm ni mshiriki mmoja katika toleo la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.
Comments