"Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri" yawakaribisha viongozi vijana wanaoshiriki katika kundi la tatu la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
- 2022-06-28 12:54:54
Leo Alhamisi, Wizara ya Vijana na Michezo imepanga ziara ya kutembelea Wizara ya Mambo ya Nje, ikiwa ni mojawapo ya shughuli za siku ya tisa ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, unaofanyika pamoja na kauli mbiu "Ushirikiano wa Kusini-Kusini na Vijana wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote", pia uko na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abd El-Fatah El-Sisi Rais wa Jamhuri kwa ushirikiano wa viongozi vijana 150 Kutoka mabara ya Afrika, Asia, Ulaya na Amerika Kusini.
Kikao cha mazungumzo kilifanyika kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu kwenye Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri, kwa mahudhurio ya Balozi Soha Gendy, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mashirika na Jumuiya za Afrika, Balozi Hazem Fahmy, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Ushirikiano wa Kimataifa na Balozi Mohamed Negm, Naibu wa Waziri wa Mambo ya Nje wa Mashirika Maalum ya Kimataifa, Waziri Mwakilishi Hassan Al-Nashar, Mhusika wa Shirika la Kimataifa la Ushirikiano wa Maendeleo, pia pamoja na mahudhurio ya Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.
Wasaidizi wawili wa Waziri wa Mambo ya Nje, Balozi Suha Gendy na Balozi Hazem Fahmy, wakati wa mazungumzo yao na viongozi vijana wanaoshiriki katika Mkutano wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika kikao cha mazungumzo kilichofanyika kwenye Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje, walieleza msimamo wa nchi ya Misri unaounga mkono masuala yote ya Afrika, Kiarabu na kimataifa na utiliaji mkazo wake wa kuimarisha Ushirikiano wa Kusini pamoja na nchi za Dunia, wakisisitiza kwamba Misri ni mojawapo ya nchi muhimu zaidi zinazoanzilisha Harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote na ina jukumu lililo muhimu ambayo inatambulika kwa kuanzisha na kuunda Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na kuiendeleza ili kuunga mkono endelevu na uhai wake kutokana na umuhimu wake mkubwa wa kikanda na kimataifa ulioisaidia kutekeleza jukumu hilo muhimu.
Katika kikao cha mazungumzo kilichofanyika kwenye makao makuu ya Wizara ya Mambo ya Nje, washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa waliuliza maswali kadhaa kuhusu mahusiano ya nchi zao pamoja na Misri na kile wanachotarajia mnamo kipindi kijacho juu ya kuimarisha mahusiano hayo ili kujumuisha nyanja mbalimbali za kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kisiasa, na wakisifu uungaji mkono wa Misri wa endelevu kwa masuala ya nchi zao, wakieleza matumaini yao ya kuongezeka mahusiano hayo na kutoa Udhamini tena na tena.
Kwa upande wake, Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , alitoa Shukrani zake za dhati kwa Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri kwa kupanga ziara hiyo na kikao muhimu cha mazungumzo miongoni mwa shughuli za siku ya tisa ya Udhamini huo katika toleo lake la tatu, na akisifu nafasi muhimu iliyofanywa na uongozi wa kisiasa wa Misri ukiongozwa na Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi Rais wa Jamhuri katika muktadha wa mahusiano yake pamoja na nchi za nje na kuwawezesha na kuwaunga mkono vijana wa nchi mbalimbali za ulimwenguni.
Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , katika toleo lake la tatu, unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa Misri wa kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kufanya kazi ya kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka Nchi zisizofungamana kwa upande wowote na wawe na maoni inayoendana na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, pia kuongeza ufahamu wa jukumu la Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote.
Comments