"Diplomasia ya Utamaduni" katika jedwali la mazungumzo la siku ya kumi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
- 2022-06-28 13:02:13
Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy, imezindua matukio ya siku ya kumi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Ijumaa hii asubuhi, kwa kikao cha mazungumzo kwa anwani ya “Diplomasia ya Utamaduni” kwa kuhudhuria Dkt. Jihan Zaki, Mjumbe wa Bunge na mwenyekiti wa zamani wa Chuo cha Sanaa huko Roma, Dkt. Magdy Zaabal, mshauri wa kiutamaduni wa zamani wa Misri huko Uzbekistan, Mbunge Hiyam Al-Khattab, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, na iliongozwa na Amir Hamza, mmoja wa washiriki wa kundi la tatu la Udhamini huo, kwa kuhudhuria Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo.
Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi na mwenyekiti wa zamani wa Chuo cha Sanaa cha Roma, Dkt. Jihan Zaki alieleza furaha yake kuwepo katika kikao hicho muhimu kwa kuhudhuriwa na vijana mbalimbali wenye tamaduni na asili tofauti wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kuwa daima anajivunia kwamba bara letu la Afrika lina uongozi katika uwanja wa utamaduni na katika maeneo ya kitamaduni yaliyoorodheshwa kwenye Urithi wa Dunia, ambayo ni maeneo yanayokuwa na umuhimu katika historia ya binadamu, kwani utamaduni sio anasa tena, bali una jukumu na umuhimu ulioifanya kuwa muhimu katika nchi zote, na kwamba Misri ina uongozi wa kitamaduni ulimwenguni na hii inapatikana katika hati za kihistoria, kwani ilikuwa mwanzo wa wazo la kuibuka na kuanzishwa kwa nchi katika ukingo wa Mto Nile, zaidi ya miaka elfu tatu kabla ya Kristo, na migawanyiko ya kiutawala na kinachofuata ilianzishwa kwenye kingo za nchi, na pia diplomasia, ingawa ni neno la Kilatini, asili yake ilikuwa kwenye ukingo wa Nile, ambapo inajumuisha wakati huo kubadilishana zawadi na kumsindikiza mgeni wakati wa kwenda nje, na wazo la kujipanga na uzalendo wake pia liliibuka kwenye ukingo wa Mto Nile, inayotuhitaji kujivunia sana kile tulichonacho kutoka kwa stoki ya kitamaduni. Na Zaki aliongeza: “Uhusiano kati ya Misri na Italia ulianza katika historia, kwani kulikuwa na maelewano makubwa ya kitamaduni kati ya nchi hizo mbili, yaliyoshuhudiwa na historia, na kulikuwa na vita vingi katika kusini mwa Saidi ya Misri na mahekalu makubwa yanayoshuhudia ushirikiano huu wa kiakili kati ya Misri na Roma, akionesha kwamba jukwaa la kwanza la kiakili la kitamaduni la Waarabu-Waafrika" likihutubia Magharibi katika nyumba zao wenyewe ni Chuo cha Sanaa cha Misri, kilichoanzishwa huko Roma mwaka wa 1926, kilichotoa picha ya Misri na Afrika ambayo sote tunajivunia, akionesha uzoefu wake katika kazi yake katika Chuo hicho, ambapo aligundua tangu mwanzo kwamba haitakuwa jukumu la kawaida, haswa kwani alipewa heshima ya kushika kiti cha urais wa Chuo kama mwanamke wa kwanza, inayohitaji kuibua jukumu la mwanamke wa Misri na Afrika na jinsi ya kuihifadhi utambulisho wake na utamaduni, akisisitiza umuhimu wa Diplomasia ya Utamaduni ambayo mara nyingi huwaokoa watu.
Mbunge Hyam Al-Tabbakh, mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, wakati wa hotuba yake katika ufunguzi wa kikao cha siku ya kumi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, aliashiria jukumu la vijana wa Misri na Bunge ya Misri katika kukarabati kada, licha ya kugusia jukumu kubwa la vijana wa Misri katika kipindi cha sasa katika kueneza diplomasia ya Misri na kuimarisha uhusiano na nchi za Afrika na nchi za Dunia, na aliongeza kuwa vijana wa Misri katika ngazi ya kisiasa ndani ya Baraza la Wawakilishi wanashiriki katika mamlaka inayohusika na uangalizi, sheria na kupitisha bajeti ya jumla ya serikali, na kwamba serikali ya Misri katika kipindi cha sasa ndani ya mfumo wa jamhuri ya kimataifa imekuwa na maelfu ya vijana katika nafasi zote za uongozi, na "Al-Tabbakh" alieleza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unathibitisha daima kuwa Misri itaendelea kuzikumbatia nchi zote zinazotuzunguka na kujali mashirikiano pamoja na nchi za Afrika, na alisisitiza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri imesababisha kuwepo kwa asilimia kubwa ya vijana katika nchi zote katika nafasi za uongozi katika ngazi ya Jamhuri, na ilishughulikia uzoefu wa Chuo cha Taifa cha Mafunzo ya Vijana na maslahi yake katika programu za vijana kwa ujumla na programu za vijana wa Kiafrika haswa, ambayo ni ukuaji endelevu. Na kuchunguza njia za kuwakilisha vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Diplomasia ya Utamaduni kwa nchi zao.
Na katika hotuba yake ya kikao cha ufunguzi wa matukio ya siku ya kumi ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Dkt. Magdy Zaabal, mshauri wa kiutamaduni wa zamani wa Misri nchini Uzbekistan, alielezea furaha yake kwa kuwepo mbele ya wasomi mashuhuri wa vijana duniani wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, na anaheshimiwa kuwa kuwepo daima katika ushiriki au tukio lolote chini ya bendera ya Kiongozi Gamal Abdel Nasser, akizungumzia uhamisho wa utamaduni wa Misri kwa jimbo la Uzbekistan, na aliona jambo hili kuwa sehemu ya fikra ya Misri katika kufikiri na utekelezaji, ambapo tunaona kuwa mwanzo wa Uhusiano kati ya Misri na Uzbekistan ulianza tangu nyakati za kale, ama katika enzi ya kisasa ulikuwa na ziara ya Rais Marehemu Gamal Abdel Nasser alikuwepo mwaka wa 1962, baada ya hapo lugha ya Kiarabu ilipitishwa kama lugha ya pili katika shule tatu kwa kwanza kama kuheshima ya ziara hiyo muhimu.
Na Zaabal alionesha uzoefu wake katika jambo hili, ambapo akifanya kazi kama mshauri wa kiutamaduni kwa Ubalozi wa Misri nchini Uzbekistan na mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Misri huko, ambapo kuzungumzia uhusiano wa kitamaduni na Uzbekistan kuna mambo muhimu, kama Misri ni suala la kiutamaduni na jukumu la kistaarabu, na kwa kutafakari historia ya Misri, tunajua kwamba ni hali ya kiutamaduni kwa sababu iliyotoa maandishi na mawazo. Na ustaarabu wa kale wa Misri ni hatua ya kwanza ya mwanadamu iliyojenga ustaarabu katika kiwango cha historia, ili kusisitiza kwamba nchi za Afrika ni miongoni mwa wana na watu bora zaidi wa ulimwengu, na huu ni uzalendo wa kihistoria na wa kistaarabu, na tunapaswa kuchukua hatua kwa msingi huu na wote ndugu katika Afrika. Na aliongeza kuwa Uzbekistan pia ni kesi ya kiutamaduni na jukumu la kiustaarabu ambapo ilipata wataalamu mashuhuri katika sayansi na kuchangia katika uzalishaji wa sayansi ya asili katika taaluma mbalimbali, wakati nchi mbili zinakutana, lazima kuwe na mwendo tofauti wa ustaarabu na utamaduni.
Mwishoni mwa kikao cha mazungumzo kilichofanyika ndani ya matukio ya siku ya kumi ya Udhamini juu ya suala la Diplomasia ya Utamaduni, washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu waliibua maswali na mijadala kadhaa juu ya suala hilo muhimu kwa vijana wanaoshiriki katika udhamini huo, huku kukiwa na mwingiliano, ukarimu mkubwa na furaha kutoka kwa kila mtu katika kikao hiki mashuhuri.
Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Bw.Hassan Ghazaly aliashiria jukumu kubwa la vijana katika kuimarisha Diplomasia ya Utamaduni, akiongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unatoa fursa sawa kwa jinsia mawili, kama inavyoonyeshwa na lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, pamoja na kuwawezesha vijana na kutoa fursa kwa wahusika kutoka nchi mbalimbali za Dunia ili kuchanganyika na kufanya mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu katika ngazi ya bara, bali hata ya kimataifa, iliyoonyeshwa na lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu.
Ni vyema kutaja kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la tatu, unalenga kuhamisha uzoefu wa Misri ya kale katika kujenga taasisi za kitaifa, pamoja na kufanya kazi ya kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka nchi zisizofungamana na maoni sambamba na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa dhana ya Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote.
Comments