"Wajumbe Vijana" watembelea Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Ustaarabu wa kimisri
- 2022-06-28 13:03:10
Leo, Ijumaa, Jumba la Makumbusho ya Kitaifa ya Ustaarabu wa kimisri huko eneo la Fustat limewapokea wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, ikiwa ni miongoni mwa shughuli za siku ya kumi ya Udhamini huo unaoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy, pamoja na Ufadhili wa Rais Abdel Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa mahudhurio ya Dk. Mustafa Waziri, katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Mambo ya Kale, Bw.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo.
Washiriki Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walikuwa wakitazama jumba la makumbusho, ambalo liko katikati ya vivutio kadhaa vya kihistoria kama vile Ngome ya Salah al-Din, mkusanyiko wa dini, na magofu ya mji wa Fustat, mji mkuu wa kwanza wa Misri ya Kiislamu.wajumbe vijana walipiga ziara kwa makumbusho , ziara hiyo ilijumuisha maelezo ya kina kwa yaliyomo ndani ya makumbusho kutoka vitu vyenye thamani na huduma zinazotolewa kutoka kwake , shughuli pekee kwa wagani wake na ambayo yamekuwa mojawapo ya makumbusho maarufu ulimwenguni , haswa baada ya tukio tofauti la kusafirisha maiti za kifalme kupitia safari yenye fahari kutoka Makumbusho ya Misri huko Tahrir.
Pia maafisa wa makumbusho wakiambatana na washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika toleo lake la tatu ndani ya jumba kuu la maonyesho na ukumbi wa wafalme Mummies ambapo walitambua vitu vya kipekee vilivyomo ndani ya makumbusho, haswa ya maiti wa kifalme, na vitu vinavyoonyesha utajiri wa ustaarabu wa kimisri na ukale wake, ambao unaoendelea hadi leo.
wakati wa ziara yao, washiriki wa toleo la tatu la Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kimataifa walielezea furaha yao kwa kutembelea Makumbusho ya Kitaifa ya Ustaarabu wa kimisri na kutazama maiti wa kifalme kwa karibu , ambao walikuwa wamefuatilia mchakato wa kuwasafirisha kwa maandamano makubwa kutoka Makumbusho ya kimisri huko Tahrir, wakibainisha kuwa walivutiwa na maiti wa kifalme, na mabaki yaliyoonyeshwa kwenye jumba la kumbukumbu yanayoonyesha ustaarabu wao wa kimisri ya kale kupitia enzi tofauti za kihistoria. vilevile , walisifu mapokezi mazuri na maandalizi ya makumbusho kwa mtindo mzuri wa kuonesha maiti wa kifalme " mummies " , na ukubwa wa Wamisri wa kale katika kuvumbua njia za kuhifadhi mwili wa maiti na hivi karibuni kwa jinsi vya kuvyotayarisha makumbusho haya , na mwisho wa ziara yako , washiriki walitilia maanani kupiga picha kadha kama kumbukumbu ya ziara hiyo .
Kwa upande wake Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa Bw. Hassan Ghazali alieleza kuwa kuandaa ziara hii kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu kwa Makumbusho ya kitaifa ya Ustaarabu wa kimisri kwa ajili ya kuwatambulisha kwa ustaarabu wa kimisri wa kale tangu zama tofauti za kihistoria na ukuu wa Wamisri wa kale unaoonekana, iwe katika mchakato wa kuhifadhi mwili au kile walichokiacha Kutoka ustaarabu mkubwa, vibaki vya kale na vitu vinginevyo , na hiyo miongoni mwa mfumo wa ziara zilizoandaliwa kwa ajili yao ambao mojawapo ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ili kujua maelezo juu ya Misri kwa karibu, ya zamani na ya kisasa.
Ikumbukwe kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , katika toleo lake la tatu, unalenga kuunda kizazi cha viongozi vijana kutoka Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote zenye maoni yanayoendana na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la harakati isiyofungamana kwa upande wowote kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo , pamoja na kuamsha jukumu la kundi wa Vijana wa Nchi zinazoshiriki katika Harakati isiyofungamana kwa upande wowote NYN na kuunganisha viongozi vijana wenye athari chanya kubwa katika upande wa nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki .
Comments