“Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa” wanahudhuria usiku wa kisanaa wa Bendi ya symphony ya Kairo

Wizara ya Vijana na Michezo, ikiongozwa na Dkt Ashraf Sobhy, siku ya Jumamosi jioni iliandaa ziara kwa wajumbe vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu kwa Nyumba ya Opera ya Misri kuhudhuria jioni ya kisanaa kwa Bendi ya Symphony ya Kairo, kwa ushiriki wa Bw. Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na kundi la Viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo.

Kwa upande wao, washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walionesha furaha yao kuhudhuria jioni hii ya kisanii ya kipekee ya okestra ya symphony ya Kairo kwenye Nyumba ya  Opera ya Misri, wakisifu jukumu la okestra katika kuimarisha maisha ya muziki nchini Misri na kwa ubora wao na sanaa yao  ya kifahari, na uangalifu wa washiriki kuchukua picha za kumbukumbu katika Nyumba ya Opera ya Misri kati ya furaha kubwa kwa uwepo wao katika nafasi hii ya kale.

Hassan Ghazaly, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alieleza kuwa ziara ya utalii iliandaliwa kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu kwa eneo la Piramidi za Giza, na imepangwa kuandaa ziara ya utalii kwa mkoa wa Aleskandaria kwa washiriki wa Udhamini huo miongoni mwa shughuli za Programu ya Udhamini ili kutambua maeneo ya utalii na ya kale ambayo Misri yajulikana kwake na ngome za ustaarabu na utamaduni wa Misri.

“Ghazaly aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa Misri katika kujenga taasisi za kitaifa pamoja na kufanya kazi ili kuunda kizazi cha viongozi wa vijana kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na maoni sambamba na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la harakati ya kutofungamana kwa upande wowote.

Comments