"Ziara ya kiutalii" huko Aleskandaria kwa wajumbe vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Leo Jumapili, Wizara ya Vijana na Michezo ikiongozwa na Dkt. Ashraf Sobhy, imeandaa ziara kwa washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, kwa Mkoa wa Aleskandaria ikiwa ni sehemu ya shughuli za siku ya kumi na mbili ya Udhamini huo unaofanyika kwa kauli mbiu “Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na Vijana wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote.” pamoja na Ufadhili wa Rais Abdel Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa kushirikisha viongozi vijana 150 kutoka Afrika, Asia, Ulaya na Amerika ya Kusini.

Wajumbe  vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, walianza ziara yao ya kiutalii huko Aleskandaria kwa kutembelea Ngome ya Wanamaji ya Qaitbay, ambapo washiriki walijua kuhusu ngome, vipengele vyake na eneo lake mwishoni mwa Kisiwa cha Pharos, magharibi mwa Aleskandaria, ambayo ilijengwa mwaka wa 882 AH, Katika nafasi ya Minar ya kale ya Aleskandaria, pia walijua kuhusu sura ya ngome, ambayo inafanana na mraba, na umuhimu wa kuta za ngome  na minara  yake ambayo ni moja ya ngome muhimu zaidi kwenye bahari ya kati.

Wajumbe Vijana hao wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, walitembelea Maktaba ya Aleskandaria, alama ya sayansi na utamaduni, ambapo walikagua maktaba hiyo na kujifunza historia ya kuanzishwa kwake na mambo muhimu ya urithi wake, ambayo inaelezea tamaduni zote, na kuifanya kuwa moja ya alama muhimu zaidi za sayansi na utamaduni katika viwango vya kikanda na kimataifa. Waandaaji wa maktaba hiyo walifanya maonyesho ya kihistoria ya Misri tangu mwanzo wa historia na matukio mbalimbali na ustaarabu ambayo ilipitia, ambayo ni moja ya nchi kubwa zenye historia na athari iliyotukuka.

Ziara ya washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, huko Aleskandaria ilihitimishwa kwa kutembelea Kanisa Kuu la Koptiki huko Aleskandaria. Washiriki walielezea furaha yao kubwa na ziara hiyo ya Aleskandaria, Bi.Harusi wa Mediterania, kuona alama zao muhimu na kufurahia hali ya hewa ya majira ya joto, Washiriki waliandika kupitia kurasa zao za kibinafsi kwenye mitandao ya kijamii, na kupiga picha na video nyingi.

Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa  Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Bw. Hassan Ghazali, alisema Udhamini wa Nasser unajitahidi kuwatambulisha vijana wa Dunia wanaoshiriki katika Udhamini huo katika maeneo ya ustaarabu wa Misri na juhudi za uongozi wa kisiasa kufikia chachu ya maendeleo katika maeneo mbalimbali. Jambo ambalo limedhihirika kupitia ziara ya Wizara ya Mambo ya Nje, Chuo cha Polisi, Bunge, piramidi za Giza na Saqqara, Maktaba ya Aleskandaria, pamoja na kutembelea baadhi ya maeneo yaliyopangwa kutembelewa, ikiwa ni pamoja na Mfereji wa Suez.

Comments