Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa katika toleo lake la tatu akutana na mshauri wa kwanza wa ubalozi wa Jamhuri ya Guinea nchini Misri
- 2022-06-28 13:10:54
Mshauri wa Kwanza wa ubalozi wa Jamhuri ya Guinea nchini Misri, Fodi Moussa Benjoura, amempokea mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la tatu, Ansuman Camara, aliyeshiriki kwa ufanisi na umahiri wakati wa shughuli za Udhamini huo, uliokuwa na kauli mbiu "Vijana wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini".
Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri iliandaa shughuli za Udhamini huo pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel-Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa kushirikisha viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, mnamo kipindi cha kuanzia Mei 31 hadi Juni 17, 2022 katika Makao ya shirika la Uhandisi huko Kairo.
Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unakusudia kuhamisha uzoefu wa zamani wa kimisri katika kujumuisha na kujenga taasisi za kitaifa, na pia kuunda kizazi cha viongozi wachanga kutoka nchi zisizofungamana na maoni yanayoendana na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza ufahamu wa jukumu la harakati ya kutofungamana kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la Harakati ya Vijana wa Nchi Wanachama katika Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote NYM, na kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa ndani ya nchi za kutofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki.
Pamoja na kutoa fursa sawa kwa jinsia zote mbili, kama ilivyoainishwa na lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, pia unawawezesha vijana na kuwapa fursa ya kujumuika na kufanya mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si barani tu, bali pia kimataifa, kama inavyoonyeshwa na lengo la kumi na saba la malengo ya maendeleo endelevu.
Comments