Balozi mdogo wa Amani...Mtangazaji wa Programu "Raia wa wa Ulimwengu mzima" Miongoni mwa orodha ya wanahabari bora zaidi Barani

"Amira Sayed" Mtangazaji wa Programu ya Raia wa Ulimwengu mzima  na Mwanachama wa timu ya kimataifa ya vyombo vya habari katika Ofisi ya Vijana ya Afrika,  mmisri wa kwanza anayepata ushirika kwa Umoja wa Afrika wa Vyombo vya Habari  baada ya ushindani mkali na wataalamu wanahabari 800, waliomba ushirika huo Barani, basi akachaguliwa ndani ya  wanahabari 15 bora kwa ajili ya kujiunga na ushirika wa kwanza wa vyombo vya habari uliozinduliwa na Umoja wa Afrika.

Amira El Sayed alianza safari yake ya kazi kama mwandishi wa habari katika gazeti "The Egyptian Gazette”, Ambapo alishughulikia mikutano mingi ndani na nje ya Misri, ikijumuisha: Kongamano la Vijana Ulimwenguni huko Sharm El Sheikh na Mkutano wa Ushirikiano wa Kimataifa nchini India,Pia alikuwa na ziara nyingi na mahojiano na waandishi wa habari na maafisa wakuu na wanadiplomasia kutoka Duniani kote, Ikiwa ni pamoja na mkutano pamoja na Naibu Waziri Mkuu, Waziri wa Mazingira na Maendeleo Endelevu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eve Baziba Masudi,na katika mahojiano na Mkuu wa Kitengo cha Waangalizi wa Uhamiaji wa Afrika, Mheshimiwa Balozi Namira Negm, na mbali na mkutano wake na mjumbe wa rais wa Marekani katika masuala ya hali ya hewa, John Kerry, na pamoja na mazungumzo yake na babake Waziri Mkuu wa Uingereza, "Stanley Johnson".

Amira El-Sayed pia alichaguliwa kama mjumbe anayewakilisha Misri katika Bunge la Dunia la Vijana la Maji, msemaji katika warsha alikuja pamoja na anuani "Usalama wa maji kufuatia mabadiliko ya hali ya hewa" Ndani ya mfumo wa matukio ya kongamano la Vijana Ulimwenguni huko Sharm El Sheikh 2018, Hii ni pamoja na ushiriki wake kama mwakilishi wa Misri katika vikao kadhaa vya kimataifa, hasa ushiriki wake katika Mkutano wa Wakuu wa Bara la Afrika nchini Niger 2019 chini ya uangalizi wa Umoja wa Afrika. Wakati huo alitunukiwa jina la "Balozi mdogo wa Amani", Kama mwanamke wa kwanza wa Misri kupokea cheo hicho, Bunge la Vijana Duniani la Maji hivi karibuni lilishiriki katika kikao kilichofanywa na Misri katika maandalizi ya Mkutano wa Kilele wa Hali ya Hewa wa COP27, na mashauriano hayo yalilenga kuzindua mpango unaounga mkono hatua za kukabiliana na hali katika sekta ya maji.

Na mnamo 2020 Mwanahabari huyo Amira Sayed amechaguliwa kama mtangazaji wa programu wa "Global Citizen Talks" ni programu ya kwanza ya vijana wanaozungumza Kiingereza iliyozinduliwa na Wizara ya Vijana na Michezo - Ofisi ya Vijana ya Afrika,na inayolenga kuunga mkono dhana ya umoja na ushiriki wa kimataifa,ikihotubia ujumbe wa kutia moyo kwa vijana wa Dunia kutoka Kairo, Kwa kuwasilisha uzoefu wenye mafanikio wa vijana duniani kote, wakati ambapo ilikaribisha idadi ya watoa maamuzi na watu wa kimataifa katika nyanja nyingi kimataifa.

Amezaliwa huko Misri ya Juu ya Misri Amira Sayed katika kijiji cha Al-Atwani, mkoa wa Aswan, na mnamo  2007, alishika nafasi ya nne katika Jamhuri katika shule ya sekondari, Kisha alijiunga na Kitivo cha Lugha na Ukalimani alihitimu mwaka wa 2012 na daraja la nzuri sana na heshima, na kwa upendo wake wa uandishi wa habari, aliorithi kutoka kwa wazazi wake,alisoma Tafsiri ya vyombo vya habari katika Chuo Kikuu cha Marekani.

Ikumbukwe kuwa ushirika wa Vyombo vya Habari vya Umoja wa Afrika sasa unafanyika Ujerumani, ndani ya muktadha wa ushirika huo, Mwandishi wa habari wa Misri Amira Sayed alitoa ripoti ya video kutoka ndani ya Ikulu ya rais, na Mbali na kuangazia hotuba ya Rais wa Ujerumani Bw.Frank-Walter Steinmeier wakati wa mkutano wake naye,pia alikutana na Waziri wa Habari na Utamaduni wa Ujerumani,Claudia Roth, pia katika ziara hiyo, alikutana na Katibu Mtendaji wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mfumo wa Kimataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi Bw. Patricia Espinosa.

Hivyo ndivyo Amira aliwakilisha mwanamke  mmisri katika vikao vya kimataifa kwa tofauti ya kipekee,isiyo na kifani, Inawakilisha raia wa kimataifa mwenye mizizi mikubwa pia thabiti , na matarajio yake ni ya juu sana hata  yanaruka kwa anga.

Comments