Sayed Megahed" mifano ya vijana wa kutia moyo kutoka kwa makada wa Ofisi ya Vijana wa Afrika
- 2022-06-28 13:13:59
"Sayed Abdullah Megahed" mwana wa mkoa wa Dakahlia, mmoja wa makada watafiti katika Ofisi ya Vijana wa Afrika, kijana ambaye anaona mwenye upole wa tabia, na bidii, uvumilivu, na taaluma mfano wa kuigwa, ama kwa sifa zake za kibinadamu, yeye ni mfano wa kuigwa katika maadili yake, anashirikiana na wengine , mshawishi, mwaminifu, na msaidizi kwa wale walio karibu naye kwa njia ya kipekee, na hata asiye na kifani.
"Megahed" alichangia kuongeza uwanja wa tafiti za kisiasa kupitia maandishi yake, michango ya kiakili, kulingana na uzoefu wake mkubwa katika uwanja wa utafiti wa kisiasa; ambapo alifanya kazi kama mtafiti katika uwanja wa mahusiano ya kimataifa, na kwake makala nyingi na karatasi za utafiti zilichapishwa miongoni mwa machapisho ya kituo cha Al-Ahram cha uchunguzi wa kisiasa na kimkakati tangu mwaka 2016, yeye pia alifanya kazi kama mtafiti wa masuala ya kimataifa katika kituo cha Nafasi ya Misri kwa uchunguzi wa kimkakati mnamo kipindi cha mwaka 2016 hadi mwaka 2018, pia alifanya kazi kama mtafiti katika kundi la taasisi ya afrika kwa ajili ya huduma ya wagonjwa wa Ini mnamo mwaka 2017, mbali na kazi yake kama mtafiti katika kituo cha vyombo vya habari kwa urais wa baraza la mawaziri tangu mwaka 2018 hadi sasa.
Mbali na hayo, "Sayed Megahed" anafanya kazi kama mtafiti wa kujitolea katika Ofisi ya Vijana wa Afrika kwenye Wizara ya Vijana na Michezo tangu mwaka 2017, hadi sasa, ambapo kupitia kwake, alishiriki katika kuandaa shughuli nyingi na mipango iliyozinduliwa na Ofisi ya vijana wa Afrika, ikiwa ni pamoja na: (Umoja wa Bonde la Mto Nile maoni ya Baadaye- Mkutano wa Kwanza wa Kairo wa kitaifa kwa vijana wa Sudan kusini - Shule ya Afrika 2063 – Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa katika matoleo yake yote matatu).
"Sayed Megahed" alihitimu katika Kitivo cha Uchumi na Sayansi za Siasa - Chuo kikuu cha Kairo mwaka 2015, kisha alipata diploma katika Sayansi za Siasa kutoka taasisi ya utafiti na uchunguzi wa kiarabu - inayohusiana na Jumuiya ya nchi za kiarabu – mnamo mwaka 2017, kisha yeye aliomba kupata shahada ya Uzamili katika Sayansi za Siasa kutoka taasisi ya utafiti na uchunguzi ya kiarabu mpaka aliipata mnamo tarehe Juni 22, 2022.
Tasnifu ya Uzamili huo ilikuja pamoja na kichwa: sera ya kigeni ya Uturuki kuelekea mgogoro wa Syria (2011-2018), ambapo alizungumzia kwa utafiti na uchambuzi maendeleo ya mahusiano ya Uturuki na Syria tangu uhuru wa Syria, pamoja na kuainisha mapinduzi ya syria kwa upande wa Asili, Maendeleo, watendaji wa kikanda na kimataifa Na jukumu la mashirika ya kikanda na kimataifa katika mgogoro wa Syria, utafiti huo pia unashughulika na msimamo wa Uturuki kuhusu mgogoro wa Syria, malengo na zana zake za sera ya Uturuki kuelekea mgogoro huo, pamoja na kushughulikia athari za sera ya uturuki kuelekea mgogoro wa Syria, pamoja na athari za sera ya Uturuki kuelekea mgogoro wa Syria na siku zake za ziazo, jambo ambalo liliifanya marejeo muhimu sana kwa watafiti, na hivyo utafiti ulipata ubora zaidi.
Hiyo ni mifano ambayo sisi tuna fahari kwa kuwepo kwao pamoja nasi, ambapo tunanufaika kutoka jaribio lao na kuchukua kutoka uzoefu wao, nasi tunasubiri kwa zaidi na zaidi kutoka kwa ubora wao huo, Mbona kutofanya hivyo!!! " Basi Mafanikio hayana mwisho, lakini mwanzo unatokana na imani kwa uwezo wako wa kufikia hilo" – Sayed Megahed
Comments