Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa akutana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa Tanzania


Mhitimu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la tatu, Mansoza Kengo, alikutana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii wa Tanzania, Dkt. Dorothy Jwajima, Naibu wake, na Katibu Mkuu wa Wizara, na baadhi ya viongozi wa Wizara hiyo, Katika Makao Makuu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Masuala ya Wanawake na Watoto, Katika mji mkuu wa Tanzania, Dodoma.


Mkutano huo ulishughulikia ufafanuzi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu,na kujadili jinsi ya kuwezesha na ya kuimarisha ushirikiano wa nchi mbili kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nyanja ya vijana, wanawake na watoto;na kujadili shughuli na programu zinazoweza kutekelezwa mnamo kipindi kijacho. 

Na Kwa upande wake, Joajima alisisitizia ushirikiano na Wizara mbili ya Vyombo vya Habari, Utamaduni, Wasanii, Michezo na ya Mambo ya Nje, kwa ajili ya kutimiza na kuamsha shughuli na masuala ya maslahi ya pamoja kwa watu wa Misri na wa Tanzania.


Na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri iliandaa matukio ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tatu, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa ushiriki wa viongozi vijana 150 kutoka nchi zisizofungamana kwa upande wowote na nchi rafiki, mnamo kipindi cha kuanzia Mei 31 hadi Juni 17, mwaka wa 2022 katika Jumba la Mamlaka ya Uhandisi mjini Kairo.


Na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa unalenga kuhamisha uzoefu mkale wa Misri katika kuunganisha na kujenga taasisi za kitaifa, licha ya kuunda kizazi cha viongozi  vijana kutoka nchi zisizofungamana zenye maoni sambamba na ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza mwamko wa jukumu la Harakati ya kutofungamana la kihistoria na jukumu lake mnamo siku zijazo, pamoja na kuamsha jukumu la k vijana wa nchi wanachama wa Jumuiya ya NYM isiyofungamana, na kuunganisha viongozi vijana wenye ushawishi mkubwa katika ngazi ya nchi zisizofungamana na nchi rafiki.


Pamoja na kutoa fursa sawa kwa jinsia mbili, kama ilivyoashiriwa na lengo la tano la Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, pia, unawawezesha vijana na kuwapa fursa kwa watendaji wa nchi mbalimbali Duniani ili kushirikiana pamoja  na kufanya mashirikiano katika nyanja mbalimbali, si tu Barani, bali ya kimataifa, kama inavyoashiriwa na lengo la kumi na saba la malengo ya Maendeleo Endelevu.

Comments