Waziri wa Vijana ashuhudia Warsha ya Mchango na Kanuni tatu za " You Think Green" Miongoni Mwa Matukio ya COY17
- 2022-11-06 17:15:14
Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ameshuhudia warsha kuhusu mchango na kanuni tatu za "Youthinkgreen", ni miongoni mwa matukio ya Kongamano la vijana katika toleo lake la 17 kwa makubaliano ya mfumo ya Umoja wa Mataifa ya mabadiliko ya tabia nchi COP17, unaofanyika mjini Sharm El Sheikh kuanzia 2 hadi 4 Novemba hii katika mji wa vijana.
Bwana Helmut Spering ambaye ni mwanzilishi "You thinkgreen International" ameendesha warsha pamoja na Bwana Thomas Frick ambaye ni mwanzilishi mwenza, Bwana Amr Selim na Ola Al Hofi kutoka timu ya" Youthinkgreen Egypt" ambapo wamefafanua mti wa matumaini na uzi wa kijani, pia shughuli kuu nchini Ujerumani, miongoni mwake maendeleo ya vijana na mawasiliano, shule ya uendelevu wa vijana ulimwenguni kama jukwaa la kimataifa na shule ya kesho.
Aidha wameweka wazi mti wa matumaini, ambapo wote wanaandika matarjio na ndoto zao wanazizotaka na kulenga mustakabali bora, endelevu na wa afya kwa vijana, pia wanashirikiana mawazo na baadhi ya majani, nayo ni ishara ya mustakbali endelevu kwa usalama na uhuru, pia ishara ya kufikiri upya na mabadiliko ya kimazingira na kijamii, na haki ziada ya kijamii ya kimataifa kuelekea njia mpya kwa maisha bora na yenye endelevu zaidi kwa wote.
Uzi wa kijani unaashiria kwamba mabadiliko ya tabianchi na kuhifadhi mazingira lazima kuwe kipaumbele cha siasa ya kijamii na uchumi kila siku.
Kongamano la Vijana la makubaliano ya mfumo wa Umoja wa Mataifa wa mabadiliko ya tabianchi COY17, linazingatiwa tukio kubwa na muhimu zaidi la vijana linasaidia kujenga uwezo na mafunzo ya siasa ili kuandaa vijana kwa kushiriki katika mkutano ujao wa tabianchi, ambapo unakusanya maelfu ya watengeneza mabadiliko kutoka zaidi ya nchi 140, inachukuliwa kuwa mkusanyiko wa vijana muhimu zaidi kwa kuzingatia wenye uwezo wa mwongozo mtazamo wa kirasmi wa vijana moja kwa moja kwenye majadiliano ya umoja wa mataifa kuhusu tabianchi, miongoni mwa matokeo muhimu ya COY17 ni hati ya kimataifa ya kisiasa ambayo imefanywa na sauti ya vijana kutoka nchi zote Duniani, itakayozingatiwa katika majadiliano ya Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi.
Inatajwa kwamba Kongamano la vijana kwa tabianchi lilifanyika pamoja na Uangalifu wa Wizara ya Vijana na Michezo na Wizara ya Mazingira, pia pamoja na usimamizi wa idara ya Jumuiya rasmi ya vijana ya mikataba ya mfumo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, na kwa msaada wa Umoja wa Mataifa nchini Misri, na idadi ya ofisi ambazo zinauhusiana kama Ofisi ya UNICEF, Mfuko wa Umoja wa Mataifa, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani, Ofisi ya UNESCO, pamoja na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kujitolea kwenye makampuni ya Misri na kwa ushiriki wa mashirika mitano ya vijana ya kimisri ( you think green _ ACTS_ Envirox_ Imam_ Vijana wapenda Misri).
Comments