Mawaziri wa Vijana,Michezo na Mazingira wakagua shughuli za mwisho kuhusu eneo la kijani
- 2022-11-06 17:17:12
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo pamoja na Dkt.Yasmeen Fuad, Waziri wa Mazingira,Mjumbe wa mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa(COP27) wameangalia maandalizi ya mwisho kwenye eneo la kijani katika kituo cha mikutano ya kimataifa ili kupokea washiriki kwenye kilele cha mkutano ya mabadiliko ya tabianchi.
Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba Misri inajali zaidi kupanua kushiriki katika Taasisi za kikanda na kimataifa za asasi za kiraia katika shughuli na maadhimisho ya mkutano wa mabadiliko ya hewa ,na kujali kwa Urais wa Misri kwenye mkutano huo kwa kusikiliza kwa sauti za asasi za Kiraia na vijana kwa mikutano kadhaa kujadili mada muhimu kwa kufanya siku yenye malengo kwao.
Dkt. Ashraf Sobhy alisisitiza kwamba eneo hilo ni maalum kwa maonesho na matukio madogo ambayo sekta binafsi uliyoandaliwa na Asasi ya kiraia , Vijana na wizara mbalimbali; kuonesha hadithi au mafanikio ya Miradi ya ubunifu na bidhaa zinazohusiana katika mapambano dhidi ya athari za mabadiliko ya hewa , pamoja na maonesho ya Muziki na kisanaa ili kuongeza uelewano kuhusu mabadiliko ya tabianchi na umuhimu wake kwa binadamu.
Kwa upande wake, Dkt. Yasmin Fuad , Waziri wa Mazingira aliashiria kwamba shughuli maalum za miundombinu na Huduma za kilojistiki zimekamilika, Huduma zote zimekamilika , Kumaliza sehemu ya mbele , na Imekamilika hivi karibuni kwa kuanzisha sehemu kadhaa ndani ya eneo la wizara ,taasisi, mashirika na taasisi za jamii ya kiraia.
Comments