Waziri wa Vijana na Michezo aangalia sehemu ya klabu za tabianchi na mazingira, pia, awasikiliza timu ya changamoto ya Vijana
- 2022-11-06 17:19:06
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliangalia sehemu ya klabu za tabianchi na mazingira, vilevile banda la msafara wa vijana na tabianchi ulioandaliwa na idara kuu ya kuuboresha uwezo wa wachipukizi kwenye eneo la burudani la kongamano hilo, pembeni mwa shughuli za kongamano la 17 la vijana la mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP27), lifanyikalo Mjini mwa Vijana kwenye Sharm El Sheikh mnamo (2-4) Novemba hii.
Sehemu hiyo inajumuisha maonesho ya bidhaa za mikoa 27 za klabu za tabia nchi na mazingira ambazo zinahusiana na kuchakata takataka, kurejesha kuzitumia na kutekeleza kazi za kisanaa kwa utumiaji wa baadhi ya aina zake, pamoja na kuonesha mitaala ya vitengo vya tabianchi katika vituo vya vijana na ambayo chipukizi waifanyia mazoezi mengi kwa awamu ya umri kuanzia miaka 8 kufikia 18, pia maonesho ya shughuli za programu "Coral" inayohusu ulinzi wa mazingira ya maji, miamba ya matumbawe na samaki, isitoshe, matukio mengi ya kutendana yanayotolewa kwa waanzilishi wa kongamano na walioshiriki kwenye banda la msafara wa vijana na tabia nchi kwa ushirikiano na UNICEF, vilevile kuonesha kwa yaliyotokea mnamo safari ya msafara kwenye mikoa tofautitofauti ya Jamuhuri.
Wakati wa matembezi yake hayo, Dkt. Ashraf Sobhy aliwasikiliza maonesho ya timu ya changamoto ya vijana wa ubunifu na kubuni masuluhisho ya kipekee kwa mabadiliko ya tabianchi, pia, kuunga mkono akili za vijana zenye mawazo mazuri na ya kimatendo kupambana na moja ya changamoto kubwa zaidi zilizowakabili vijana hawa.
Timu ya changamoto ya vijana, katika onesho lake, ilizingatia masuluhisho ya mabadiliko ya tabianchi yanayochangia malengo ya maendeleo endelevu kwa ushirikiano wa vijana 8000 (Wavulana na Wasichana ) kutoka mikoa mbalimbali, pia, timu tano zilichaguliwa kama miradi bora zaidi kutatua masuala ya tabia nchi, aidha, kuwawasilisha washindani wawili bora shindano la kimataifa, kwa vile walichaguliwa kati ya miradi 30 yenye ubora kutoka jumla ya miradi 71 ya wanaoshindana katika shindano la kimataifa.
Kongamano hilo linafanyika kwa uangalizi wa Wizara ya Vijana na Michezo na ya Mazingira, vilevile kwa usimamizi wa idara rasmi ya mzunguko wa vijana kwa mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, kwa uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa nchini Misri na idadi ya ofisi zake kama ofisi ya UNICEF na shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu, programu ya maendeleo ya Umoja wa Mataifa, Shirika la Afya Duniani, ofisi ya UNESCO, pamoja na shirika la kitaifa la uhamiaji, ofisi la wanaojitolea wa Umoja wa Mataifa na ofisi ya mkataba wa kimataifa wa Umoja wa Mataifa kwa ushiriki wa kimisri na ushirki wa mashirika matano ya vijana ya kimisri (you think green, acts, environics, El emam, vijana wanapenda Misri)
Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba mpango wa changamoto ya vijana ni miongoni mwa juhudi zinazofanywa na Wizara ya Vijana na Michezo ili kuwatayarisha vijana na kuwawezesha ushiriki wa kimatendo kufikia malengo ya maendeleo endelevu na ajenda ya Misri ya 2030, vilevile ni kati ya mpango wa nchi kuwawezesha vijana na chipukizi kufikia masuluhisho kwa matatizo yanayoyakabili mazingira, na kushiriki kwao kwa ufanisi ni miongoni mwa juhudi za kimataifa kukabiliana na suala la mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya kuchangia uokoaji wa mfumo wa kiikolojia na jaribio la kuhakikisha mustakabali bora zaidi ya maisha.
Meja Jenerali Ismael El Far, kiongozi wa sekta ya vijana, Dkt. Amr El Hadad, naibu Waziri huyo kwa maendeleo ya kimchezo, Azza El Dry, Mkuu wa Idara kuu ya kuboresha uwezo wa chipukizi, Manal Gamal El Din, Mkuu wa Idara kuu ya kuwawezesha vijana na Eman Othman, msimamizi mkuu wa idara kuu kwa wenye vipawa na wabunifu, wote walimwandamana Waziri wakati wa kuangalia kwake maonesho hayo.
Comments