Mmisri "Hassan Ghazaly" ashinda Tuzo ya Afrika ya kuacha Athari za Kijamii na Maendeleo ya Vijana kwa 2022

Kiongozi kijana wa Misri, Hassan Ali Ghazaly, mtafiti wa masomo ya Anthropolojia, mtaalamu wa sera za  vyombo vya habari na vijana, pia ni mwanaharakati katika nyanja za diplomasia ya vijana na utamaduni, alipokea Tuzo ya Afrika kwa kuacha Athari za kijamii na Maendeleo ya Vijana huko Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayotolewa na Kituo cha Maendeleo ya Uongozi na Ujasiriamali Afrika PALEDEC, nasi tunakuta  Mtafiti Menna Yasser, na mwanaharakati Fillion Henry, Viongozi Vijana wawili mashuhuri, wahitimu wa Udhamini wa  Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa waliipokea kwa niaba yake, , ambao ni wanachama wa Harakati ya Nasser ya Kimataifa kwa Vijana nchini Tanzania, na hiyo ilikuja wakati wa Mkutano wa Saba wa Uwekezaji wa Afrika, ulioanza jana jioni, Jumanne, Novemba 8, Kwa mahudhurio ya viongozi 350 wakiwemo kundi la wafanyabiashara mashuhuri, viongozi na wawakilishi wa Jumuiya na taasisi za vijana katika ngazi ya kimataifa kutoka nchi takriban 42 Duniani, pamoja na uongozi wa Dkt.Hussen Ali Mwinyi, Rais wa Kisiwa cha Zanzibar na Bw. Danny Faure, aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Ushelisheli.


Wakati wa mazungumzo yake, Ghazaly alielezea furaha yake kubwa kwa kuchaguliwa na kamati ya tuzo kama mmoja wa viongozi mashuhuri vijana kijamii na kimaendeleo katika ngazi ya duru za vijana wa Kiafrika, akibainisha kuwa anaichukulia heshima hii na kutawazwa kuwa ni jukumu zuri  linalobeba dhima kubwa zaidi kwa wenzake kuanzia vijana wa bara hili, na hata kilele cha nafasi ya Misri katika duru ya Afrika katika kipindi chote cha upanuzi wake tangu mapinduzi ya Julai 1952, na kusababisha miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa kati ya nchi hizo mbili, kama vile Bwawa la Nyerere, ambalo Misri inalijenga nchini Tanzania. Hivi majuzi,  inayothibitisha umakini wa Misri kwa maendeleo halisi ya watu waafrika bila madhara, Bila ubaguzi, na pia kuashiria kwamba tuzo hiyo inaweza kuchukuliwa kama aina ya kuimarisha viunganishi vya nchi hizo mbili, Misri na Tanzania, akisisitiza kwamba ataendelea na kazi yake kwa usaidizi na uangalifu zaidi, na kufanya kazi ya kuhamasisha viongozi zaidi wa vijana ili kuendeleza bara na kuinua hadhi yake, kwa kuzingatia dhana ya uwajibikaji wa kijamii na kuamini nguvu za vijana na kuwekeza ndani yao, kufikia kesho yenye mafanikio.


"Ghazaly” ana taaluma tajiri ya zaidi ya miaka kumi na motatu, kwa kijana asiyezidi miaka thelathini na mitano, ana maoni tofauti na ya kipekee, na uzoefu mzuri sana na ujuzi na changamoto, na athari kubwa ya kijamii katika viwango vya kindani na kimataifa, Wakati huo alianzisha miradi na programu kadhaa za kitaifa, za Kiafrika na kimataifa zinazohusika na maendeleo na uwezeshaji wa vijana na uimarishaji wa uwajibikaji wao wa kijamii kwa nchi zao. Miongoni mwao ni Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na mpango Afromedia , Shule ya Kiangazi ya Kiafrika, na mradi wa "Umoja wa Bonde la Nile - Maoni ya Baadaye", na Mfumo wa Uigaji  wa AU, Harakati ya Kimataifa ya Nasser kwa Vijana, na njia zingine za kijana huyu, zina ushawishi mkubwa kwa duru za vijana wa Kiafrika na kimataifa, ambao wana kauli mbiu "Misri ni kijiji changu ... Afrika ni nchi yangu."



Ikumbukwe kuwa Kituo cha Maendeleo ya Uongozi na Ujasiriamali Barani Afrika PALEDEC ni asasi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2015, kwa lengo la kufanyia kazi ya ustawi wa Bara la Afrika kwa kurahisisha mahusiano ya muda mrefu na mipango ya kimkakati itakayoongeza fursa za biashara na uwekezaji, kiliweza mnamo miaka saba utekelezaji wa miradi zaidi ya 41 katika nchi 21 za Afrika zikiwemo Nigeria, Zimbabwe, Zambia, Kenya, Uganda, Ghana, Senegal, Liberia na Cape Verde, Na kuzindua takriban mikutano saba ya kilele ya kiuchumi iliyoandaliwa na Dubai, Dar es Salaam, Rabat na Abu Dhabi, iliyohudhuriwa na washiriki wapatao 7800, kwa kujadili masuala ya pamoja ya kiafrika kwa nia ya kutoa mtazamo mpana, wa .kibunifu na wenye nyanja nyingi kama vile maendeleo ya kijamii na kiuchumi na maendeleo endelevu Barani Afrika.

Kituo hicho pia kinazindua tuzo ya kila mwaka katika Sehemu kadhaa, ikiwa ni pamoja na ujasiriamali, uwezeshaji wa wanawake, ujenzi wa ushirikiano, maendeleo ya vijana na athari za jamii, maendeleo ya kiuchumi, kujenga amani, Hadi sasa, imepatikana na watu takriban 92, wakiwemo viongozi wa serikali, wafanyabiashara, wawakilishi wa jumuiya na mashirika ya vijana, na wawekezaji kutoka nchi 45 za ndani na nje ya Afrika.

Comments