Waziri wa Vijana ashiriki katika kikao cha " Vijana na mabadiliko ya Hali ya Hewa" katika mahali pa Shirikisho la Benki za Misri
- 2022-11-12 20:54:36
Sobhy: fursa za Vijana katika Ufadhili ziliongezeka kwa kiasi kikubwa mnamo siku za hivi karibuni.
Taasisi za Ufadhili zinapaswa kutafutia miradi mipya ya kimichezo ya Vijana, pia inayoshughulikia sekta ya Hali ya Hewa na kupanua Ufadhili.
Dokta Ashraf Sobhy,Waziri wa Vijana na Michezo alishuhudia kikao cha " Vijana na mabadiliko ya Hali ya Hewa" kwenye makao makuu ya Shirikisho la Benki za Misri,miongoni mwa Vikao vya Siku maalum ya Vijana na vizazi wajao, inayoandaliwa miongoni mwa shughuli za toleo la 27 kwa Kongamano la pande kadhaa kwa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kwa COP 27 ( Mabadiliko ya Hali ya Hewa) ambayo shughuli zake zinaendelea hadi 18 Novemba hii mjini mwa Sharm ElShekh.
Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba Mkakati wa Wizara unalenga kujenga uwezo wa Vijana wa Misri na kuwasaidia kijamii na kiuchumi, pia Kueneza utamaduni wa ujasiriamali, miradi huria na miradi midogo na ya kati ,ili kupatia mapato ya kutosha na endlevu,na kusimamia uwekezaji na akiba kwa Vijana kupitia benki za kitaifa zinazolenga kuongeza maisha ya watu na kudumisha maisha bora na kuzidisha viwango vya Ushirikishaji wa Fedha na Shughuli za kifedha mbalimbali, kwa njia sambamba na kuunga mkono mkakati wa kitaifa wa Misri 2030.
'Sobhy' aliongeza kwamba pia mkakati unalenga kuwapa Vijana nafasi sawa kuwa wenye ushawishi katika jamii ya Misri,na kuongeza kiwango chao cha fahamu kuhusu changamoto na hatari zinazokubaliana uchumi wa Misri ,na kuongeza ufahamu kwa athari za uvumi kuhusu Usalama wa Taifa، na umuhimu wa hili katika kufikia ushirikishaji wa Fedha inayolenga pia kusaidia matabaka yote ya kijamii kufikia bidhaa na huduma za kifedha zinazokidhi mahitaji yao mbalimbali.
Waziri huyo aliashiria ushiriki wa benki za kitaifa katika uanzishaji wa sanduku la hisani kusaidia Michezo ya Misri,na pia aliashiria ushirikiano kati ya Wizara ya Vijana na Michezo na benki kadhaa kuanzisha matawi ya benki hizi ndani vituo vya vijana na mashirika ya vijana ,na kupatikana mashine za ATM katika vituo vya vijana walengwa.
Dokta Ashraf Sobhy alidokeza kuangalia Programu kadhaa kwa ajili ya kueneza Utamaduni na Ushirikiano wa Fedha, nazo ni kama: kuunga mkono Wafanyabiashara wadogo na wa kati miongoni mwa mpango wa "Viongozi wa Nile " pamoja na Ufadhili wa Benki Kuu ya Misri, ambapo mpango huo unalenga kutoa msaada kwa Vijana Wajasiriamali na Kuhimiza makampuni changa katika sekta mbalimbali za kiuchumi kwa kutoa misaada kwao.
'Sobhy' aliomba taasisi za kiufadhili kwa dharura ya kutafutia miradi mipya ya kimichezo ya Vijana inayoshughulikia na sekta za hali ya hewa na kupanua ufadhili, akiashiria kuwa nafasi za Vijana katika ufadhili ziliongeza kwa kiasi kikubwa mnamo siku za hivi karibuni.
Mkutano huo ulihudhuriwa na:
-Sherif lokman,Naibu Mkuu wa Benki Kuu kwa ushirikishaji wa Fedha,na -Tarek Fayed ,Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Kairo,
-Ahmed Sabah,Mkurugenzi Mkuu na Mshiriki mwanzilishi wa Kampuni yaTilida,
-Seif Salama،Meneja wa Uendeshaji katika mashamba ya Tolema,
- na Bibi/ Klimons Fedal , Meneja wa Ofisi ya Shirika la Maendeleo la Ufaransa nchini Misri.
Comments