Waziri wa Vijana na Michezo akutana na Mkurugunzi wa Ushirikiano katika Taasisi la kimataifa la Skauti


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo     alikutana na Mkurugunzi wa Ushirikiano katika Taasisi  la kimataifa la Skauti, Bi. Hana Graham, pembezoni mwa mkutano wa nchi husika katika mkataba wa mifumo kadhaa kwa mabadiliko ya  hali ya hewa  Cop27;  kujadili  kuimarisha Ushirikiano wa pamoja mnamo kipindi kijacho, pia kuzungumzia matayarisho ya Misri ya kupokea Mkutano wa kimataifa wa Skauti, Na. 43,utakaofanyika mwaka wa 2024 mjini Kairo.


Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo amethamini juhudi zinazofanywa kutoka kwa Taasisi ya kimataifa ya Skauti, akisisitiza umuhimu wa  Skauti ya Misri ndani ya Harakati za Skauti, kama harakati moja  muhimu zaidi na kale pia kwa Vijana wa Misri, ambazo zilianzishwa tangu zaidi ya miaka 100 haswa huduma zao za kudumu kwa nchi  wakati wa migogoro.


Sobhy, ameeleza kuwa Ilikuwa kuliomba msaada wa kundi la Skauti  nchini Misri, wakati wa  janga la virusi vya Corona na miradi ya  maendeleo na  masuala ya mazingira, miongoni mwa mipango ya Taasisi ya kimataifa ya Skauti ili kutekeleza malengo ya maendeleo endelevu.


Bi. Hana Graham, ametoa Shukrani  kwa Waziri wa Vijana na Michezo kwa  juhudi zake zinazofanywa katika matayarisho ya mkutano wa kimataifa wa Skauti, Na. 43, utakaopangwa kufanyika mwaka wa 2024 mjini Kairo, kama Jumuiya kuu kwa viongozi wote wa Jumuiya za Skauti za kitaifa Duniani kote, pia kumshukuru kutoa aina zote za misaada kwa Mkutano wa kiarabu wa Skauti,Na.29, unaofanyika huko Sharm El Sheikh mnamo 2019.


Mkutano huo ulihudhuriwa na Mustafa Magdy msaidizi wa Waziri kwa Sera  na maendeleo kwa Vijana, pamoja na  kundi la wanachama wa bodi ya Chama kikuu cha Skauti, wanachama wa kamati ya masuala ya nje kwa Chama kikuu cha Skauti, na Marwan Ahmed Awny, mtafiti wa Shirikisho la Sera na kuboresha shughuli.

Comments